MUNGU wetu ni mkuu, jina lake ni kuu , uweza wake ni mkuu na matendo yake ni makuu.

Moto unawaka sasa, moto ni damu ya YESU KRISTO. Moto huu ukishuka watu hufunguliwa na kuwa wazima kabisa.
BWANA YESU asifiwe.
 Leo katika ibada Maisha ya ushindi blog tulikuwa Kawe Pentecostal Church kwa mchungaji Elly Boto.

MUNGU humtumia sana mtumishi wake huyu kwa kuwafungua watu kutoka katika kila aina ya vifungo vya shetani.

Ndugu kama unahitaji maombi au ushauri wa kiroho mpigie mchungaji Elly Boto kwa namba 0719640642 au 0752965812. pia unaweza kumpigia mzee kiongozi wa kanisa hilo kwa namba 0657361222. ni bure kabisa 

MUNGU wetu ni mkuu, jina lake ni kuu , uweza wake ni mkuu na matendo yake ni makuu.

 hizi ni baadhi ya picha wakati wa maombezi kanisani hapo.


Ukombozi ukifanyika kwa jina la YESU KRISTO.

Dada huyu baada ya kuteseka sana hatimaye akimbilia uzima kwa YESU KRISTO, Hapa akiombewa na Mchungaji Elly Boto..



Dada huyu akishukuru kwa BWANA YESU kumponya kupitia maombi kanisani KPC

Baaba ya kuombewa na kupona , ndugu hawa walitoka mbele na kuanza kushuhudia matendo makuu ya MUNGU aliyowatendea.


Comments