MWIMBAJI HEKIMA KWAYA KINONDONI AFARIKI

Mwanakondoo ameshinda,Tunasikitika kutangaza kifo cha mama Yetu Mpendwa (Mama Mwambepo) kifo chake kimetokea usiku wa kuamkia leo. 
 
Alikuwa ni mwimbaji wa kwaya kuu hapa Kinondoni. hakika hili ni pigo kwa kanisa ila maandiko ya Mungu yananena wazi kuwa imetupasa kushukuru kwa kila jambo. 
 
Nasi hatuna budi kurudisha sifa kwa Mungu wetu aliyehai. Uongozi wa Hekima kwaya na Waimbaji kwa ujumla wao wanatoa pole kwa familia ya marehemu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen
Mama Mwambepo (wa pili kutoka kulia waliochuchumaa, enzi za uhai wake akiwa na waimbaji wenzake wa Hekima kwaya kinondoni)

Comments