NYOTA WA MUZIKI WA INJILI NCHINI KENYA AFARIKI DUNIA


Mwimbaji wa muziki wa injili nchini Kenya aliyetamba na wimbo wa 'Kiburi ni chanini' aitwaye Peter Kahura Kaberere amefariki dunia baada ya kupigwa shoti ya umeme akiwa kwenye eneo lake la kusafisha magari siku ya jumapili.

Mwimbaji huyo ambaye pia alikuwa meneja wa kampuni ya Mo Sound Limited ambayo pia inasimamia tuzo maarufu za nchini humo za Groove, alipatwa na umauti wakati akisafisha gari lake tayari kuelekea kanisani eneo la Lower Kabete lakini kukawa na hitailafu ya umeme kwenye mashine ya kuoshea gari  ambayo ilisababisha umeme huo kumkausha na kukutwa sakafuni na mkewe akiwa amekufa.

Taarifa za kifo cha mwimbaji huyo zilitolewa na mkewe kupitia ukurasa wa Facebook wa mwimbaji huyo na kufuatiwa na salamu mbalimbali za rambirambi kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wapenzi wa muziki wa injili. Taarifa hizo ziliendelea zaidi kupitia ukurasa wa Facebook wa tuzo za Groove ambao pia ujumbe wao uliandikwa kuonyesha ni kwa jinsi gani wamehuzunishwa na kifo cha mwimbaji huyo.






Mwili wa mwimbaji huyo upo nyumba ya kuhifadhia maiti ya Lee funeral home ikisubiriwa uamuzi wa mazishi kutangazwa na familia yake. Peter alinza uimbaji wake kupitia kundi la Zaidi ya muziki kisha kujitoa na kuwa mwimbaji wa kujitegemea ambapo aliwahi kumshirikisha mwimbaji kama Eunice Njeri kupitia wimbo wake wa Natamani, Just A Way aliomshirikisha Mr Vee pamoja na wimbo mwingine uitwao Mwanamke aliomshirikisha Bechani. Marehemu ameacha

   "BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE"


Peter na familia yake enzi za uhai wake
Chanzo ni Gospel kitaa

Comments