Rudi katika Nafasi yako uliyowekwa na Mungu

  Kutana na Mtu wa Mungu  Nabii Samson  pale katika hema ya Kinabii Geita kwaajili ya kufunguliwa kukombolewa kuwekwa huru kurejeshwa, kwa msaada zaidi piga simu ni Bure 0756 809 209 Mtu wa Mungu,
 
Utangulizi:
Mambo yanayofanyika siku za leo kote ulimwenguni ni Dalili halisi za kuonyesha kuwa kanisa la kristo alilokusudia liwepo Duniani limehama katika nafasi yake, na Muovu  ametumia nafasi hiyo kufanya kila jambo analolitaka kutimiza kusudi lake na yeye,

Kanisa ni nini:
Tafsiri ya kanisa imetafsiriwa na watu mbali mbali kwa mitazamo tofauti na mafunuo tofauti lakini katika hayo yote majibu halisi yanatoka kwa mwenye kanisa ambaye ni Yesu Kristo ndiye anayeweza kutuambia kanisa ni nini, tuangalie maneno yake mwenyewe juu ya kulijenga kanisa lake,
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Mathayo 16:18,matendo 13:1,14:27,15:4 18:22

Sasa tumejifunza kwamba kanisa ni mtu aliyetayari kutumika na Mungu aliye imara si kigeu geu, leo yupo kwa Mungu  kesho Kwa wachawi kesho , wewe ni wadhamani sana, hebu tuangalie mfano mwingine juu ya kanisa
Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa Gerezani. Matendo ya mitume 8:3

Maandiko yote mawili yanadhibitisha kuwa Kanisa ni wewe na siyo jengo ila jengo linapata heshima baada ya wewe kukusanyikia humo sasa umenielewa kwamba nikisema rudi katika nafasi yako  Ninamaanisha turudishe kanisa mahapi ambapo kiristo aliliweka, kumbuka niwapi  Yesu amekuweka, ili urudi hapo haraka    kabla gadhabu ya Mungu haijawaka juu yako,
Nini Ufanye ili kurudi katika nafasi yako,
Agizo langu ninawakumbusha agizo nililopewa na Mungu juu yako,
Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama vile nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa.1wakorintho 4:17

Namna pekee ya kurudi katika nafasi zetu ni toba ya kweli  juu ya njia tulizozichagua  sisi wenyewe tukaiacha njia ya uzima tukaifuata njia ya mauti, kanisani unakuja lakini dhambi hutaki kuacha, umechaguwa mauti ya umilele  Dhambi ni njia ya mauti, uwongo,uchawi,kuabudu sanamu,kuzini,kuzusha,uwoga,mizaha,

Na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. LUKA 24:47

Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. Matendo ya mitume 20:28
Tumelipiwa gharama kubwa sana ambayo hakuna Mtu aliye na uwezo wa kuilipa hivyo tusichezee uwokovo tulionao ni ghali mno,
Piga magoti anza kutubu, na kukiri makosa juu ya toba
  ( marko 8:18 )wana macho lakini hawaoni wana masikio lakini hawasikii,wana akili lakini hawakumbuki lolote, tumepitishwa katika mateso mengi bila ya kujuwa wala kuona  maana tulitekwa sasa basi, leo mwisho warumi 8:1-6  Nahumu 1:9 Unawaza nini juu ya bwana ili akomeshe mateso yako ili yasirudi kwa mara ya pili,

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
 Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.
Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.

Nami nitaonekana kwenu, asema Bwana, nami nitawarudisha watu wenu waliofungwa, nami nitawakusanya ninyi, nikiwatoa katika mataifa yote, na katika mahali pote, nilikowafukuza, asema Bwana; nami nitawaleta tena, hata mahali ambapo kutoka hapo naliwafanya mchukuliwe mateka. Yeremia 29:11-14

Dhambi zinapofusha macho zinaleta ukiziwi akili zinakamatwa haziwezi kukumbuka lolote, Mungu atusaidie sana,

kusimama katika nafasi,

Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu.
Habakuki 2;1
Ndipo akalia kama simba, Ee Bwana, mimi nasimama daima juu ya mnara wakati wa mchana, na kila usiku ninakaa katika zamu ya ulinzi wangu.
Isaya 21 : 8

Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari.
Mathayo 14 : 25 
Ukiwa katika nafasi yako yesu atakukuta hapo hapo usikimbie tatizo lililo mbele yako Yesu anakuja siyo kivuli chake,

Comments