SOMO: KUBADILI MWENENDO WETU( Sehemu ya 2)



Wapendwa katika KRISTO YESU somo hili linaendelea, na leo tuangalie.. 

 TUFANYEJE ILI MIENENENDO YETU IWE MIZURI?,

Mtumishi Alex
 Ili mienendo yetu iwe mizuri ya kumpendeza Mungu ni lazima kuacha DHAMBI/MAOVU NA KUOMBA REHEMA MBELE ZA MUNGU! "1Yoh 1:8-10 Biblia inatuambia kwamba tukisema kwamba hutuna dhambi tunajidanganya wenyewe na wala kweli haimo ndani mwetu, lakin tukiziungama dhambi zetu yeye ni mwaminifu atatuondolea dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote, pia anasema tukisema kwamba hatujatenda dhambi tunamfaoya Mungu kuwa mwongo..

 "Mithali 28:13 Biblia inasema yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.. 

"ISAYA 43:25 Mungu anasema kwamba yeye ndiye ayafutaye makosa yetu na wala hatakumbuka dhambi zetu., Pia unaweza kusoma ZABURI 32-1-6. Kwa hiyo basi unaweza kuona ni kwa jinsi gani "TOBA" ilivyo na nguvu ktk kubadili mienendo michafu. 

SILAHA KUU 3 ZINAZOWEZA KUSAIDIA ILI MWENENDO WETU UKAE SAWA SAWA NA MUNGU!,

 Silaha hizo ni 

(1)NENO>>Yoh 8:31, Yakobo 1:21, Zabur 119:11, Zabur 107:20.

 (2)IMANI>>Waibrania 11:1, Waibrania 11:6, Waibrania 10:38.

 (3)MAOMBI>>Mithali 8:17, 2Nyakati 7:14. 

Hizi silaha zina nguvu sana ktk ulimwengu wa roho ili kumsaidia mtu mwenendo wake ukae sawa sawa na Mungu, kwa IMANI, NENO, na MAOMBI tutaweza kumshinda shetani pamoja na matendo yote ya giza, hizi silaha zote zinaendana kwa wakati mmoja, ukipungukiwa moja kati ya hizi imekula kwako, shetani atakugalagaza kama apendavyo. --MWISHO WA SOMO HILI--, Napenda kuwashukuru wale wote mliochukua muda wenu kulifuatilia somo hili mpaka mwisho Mungu awabariki sana, naamini kuna kitu utakuwa umejifunza!, Mwisho "MIENENDO YOTE MICHAFU AMBAYO HAIMPENDEZI MUNGU MWISHO WAKE NI JEHANAMU KTK LILE ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI. Ufunuo 21:8"

MUNGU awabariki sana.
By Alex wa Yesu.

Comments