SOMO: KUBADILI MWENENDO WETU!

Karibu mwana wa ufalme ufuatane nami ktk somo hili na Mungu akubariki. 

Ninaposema KUBADILI MWENENDO namaanisha kwamba ni kugeuka/kugaili na kuacha maovu/dhambi pamoja na mambo yote ya kidunia ambayo hayampendezi Mungu na kumrudia Mungu ili uendelee kuishi maisha matakatifu. je biblia inaeleza nini juu ya hili. 

"EFESO 4:17-32" Biblia inaeleza jinsi mwenendo watu unavyotakiwa kuwa kwamba tusiwe kama watu wa mataifa wanavyoenenda bali tubadili mwenendo wetu yaan utu wa zamani ili roho zetu zifanywe upya kwa kuuvaa utu upya unaopatikana ktk haki na utakatifu.

 Na Mtumishi wa MUNGU,Alex.
 "1PET 4:2-5" Biblia inatueleza kubadili mwenendo wetu tutoke ktk tamaa za wanadamu ili tuweze kujua mapenzi ya Mungu kwan muda wetu iliobaki ni mchache, pia tunaambiwa kuacha mienendo mibaya kama ufisadi, ulevi, tamaa, karamu za ulafi, vileo na ibada ya sanamu. Mpendwa ktk KRISTO YESU karibu tena ktk somo hili ili tuweze kuendelea, kama tulivyoangalia jana baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuchafua mienendo yetu na kututenga na utukufu wa Mungu, mambo haya ni vyema kuyaacha ili mienendo yetu ikae sawa sawa na Mungu wetu. 

"KOLOSAI 3:5 Biblia inaeleza matendo machafu ambayo yanaweza kuchafua mienendo yetu sisi kama watu tuliokoka, mambo hayo ni kama uasherati, tamaa mbaya, mawazo mabaya, hasira, uongo, matukano na matusi, hivyo tunaambiwa kubadilika na kuvaa utu upya ili tupate ufahamu sawa sawa na mfano wake aliyetuumba. 

"2TIMOTHEO 2:22 Biblia inatuambia kwamba tukimbie tamaa za ujanani ili tutafute haki, imani, na upendo na amani, kumbe ili tupate amani, upendo, haki, na imani ni lazima tubadili mienendo yetu michafu.

 "1YOH 2:15-17 Biblia inaeleza kuhusu kumpenda Mungu, kwamba kama unataka kumpenda Mungu lazima tuachane na mambo ya dunia Na kama tutaipenda dunia haiwezakani hata kidogo kumpendeza Mungu. 

"WARUMI 12:1-2 Neno la Mungu linatukumbusha kuitoa miili yetu kuwa dhabihu iliyo hai na kugeuzwa upya nia zetu ili tuweze kujua mapenzi ya Mungu yaliyo mema. 

"WARUMI 6:12 Biblia inaeleza kuhusu dhambi, dhambi ambayo ikimtawala mtu hali yake huwa mbaya na mtu huyu hujikuta akizitii tamaa zake. pia biblia inasema tusivitoe viungo vyetu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi bali inatakiwa tujitoe kwa Mungu kama tulio hai, na hii itawezekana kama tutabadili mienendo yetu ya dhambi na kufikiria toba ambayo ndio msaada.

 "WAEFESO 5:1-12 Biblia inaeleza mambo mengi hapa ambayo inapaswa tuyaache sisi kama waenda mbinguni, mambo hayo ni kama uasherati na mambo mengine mengi, pia biblia imesema vizuri hapa kwamba hakuna mwasherati wala mwenye tamaa aliye na uridhi ktk ufalme wa Mungu.Wapendwa somo hili linaendele, leo tuangalie.. 

JE NI KWANINI TUNABADILI MIENENDO YETU?

 (1)ILI TUPATE KUMPENDEZA MUNGU NA KUISHI MAISHA MATAKATIFU-->Zaburi 16:3, Walawi 11:44-45. 

(2)ILI MUNGU AENDELEE KUONEKANA NA KUJIDHIHILISHA KTK MAISHA YETU-->Zaburi 50:23, Yoh 14:21, Mathayo 5:8, 2Nyakati 7:14. 

(3)ILI TUPATE KUULITHI UZIMA WA MILELE YAAN TWENDE MBINGUNI-->Efeso 5:1-5, Mathayo 19:27-29, Galatia 5:19-21, Ufunuo 21:27, Ufunuo 22:14,

 (4)ILI MUNGU AENDELEE KUWEKA ULINZI JUU YA MAISHA YETU-->Zabur 34:7, Zabur 27:1-5, Mithali 3:21-26, Mithali 2:7-8, Nahumu 1:7. 

 (5)ILI MUNGU AENDELEE KUTUINUA NA KULETA BARAKA KTK MAISHA YETU-->Ayubu 8:5-8, KUM 28:1-8, KUM 11:13-15. 

Hivyo basi hatuwezi kupata mambo haya 5 kama mienendo yetu itakuwa michafu. lazima mienendo yetu ibadilike iwe yenye kumpendeza Mungu..

MUNGU akubariki sana.
SOMO LITAENDELEA.
By Alex wa YESU.

Comments