TANZANIA PASIPO WOKOVU IMEKUFA!

Dar es salaam


Bwana Yesu asifiwe...

Sasa ili sijui niliite ni somo au fundisho? Ahaa mimi sijui bhana!
Lakini ngoja niseme kidogo tu,yaani kidogo tu,juu ya Tanzania yangu,nchi niipendayo. Ninachowiwa ndani yangu kukisema ni hiki hapa kidogo;

Tanzania ni miongoni mwa nchi iliyokuwepo katika mikono ya nguvu za giza zito.Ila Mungu akaipenda hata kuwaweka watu wake waende kuisafisha kwa uweza wa jina la Yesu Kristo wa Nazareti.Leo hii,jinsi unavyoona amani usifikiri ilikuja yenyewe Bali walikuwapo watu wa Mungu waliolia kwa ajili ya Tanzania.

Nami nakaza kusema;
Tanzania kama si walokole wenye kuiombea usiku na mchana na iseme sasa.
Ukweli wenyewe ndio huu;
Watu waliokoka Tanzania wana nafasi kubwa sana kuifanya Tanzania kuwa Tanzania sababu jicho la Mungu Baba li ndani yao.

Miaka michache iliyopita walokole tulikuwa hatuthamaniki kabisa. Ilikuwa ni vigumu kumuona mlokole akishika wadhifa mkubwa serikalini au kwenye mabenki,Ila hali ya sasa ni tofauti na miaka ya zamani.
Mungu kashusha wokovu wake ulio mkuu kiasi kwamba kila nafsi isipotee ifikirie toba,na KUOKOKA.

Leo wapo wakurugenzi wengi tu,wakutosha,wale waliokoka.Mameneja mbali mbali wa taasisi za uma na za kiserikali,wengi wameokoka,ni Haleluya tu.

Siku moja nilipokuwa katika bank moja ya kibiashara Tanzania,nikaonana na branch manager,alikuwa ni mdada furani hivi mzuriii,kumbe uzuri wa yule dada ulikuwa ni WOKOVU.Alikuwa ameokoka kupitiliza,nami nikashangaa kidogo,kumuona jinsi alivyo na hata nafasi aliyokuwa nayo.

Ndiposa nikasema msalaba mbele dunia nyuma!
(The cross before me,the world behind me)

Haleluya....

Mpaka mimi huwa ninaona kwa nini serikali yetu isitutengenezee kajumba kadogo maeneo ya ikuru hivi,au ndani ya hospitali ya taifa Muhimbili kisha walokole wenye upako tukawa huko kuwaombea viongozi wetu kwa kuwawekea mikono,au kuwafungua wagonjwa tukiwa katika kajumba chetu cha maombi hospitalini.
Lakini haya ni mawazo yangu!

Leo;
Kuna wabunge wengine ni wachungaji ni Haleluya tu....safi kabisa.Hawa ni wafua chuma waliotumwa na BWANA Mungu kuziangusha pembe zote za yule mwovu (Zekaria 1:18-19)

Wito wangu kwako ni huu;
*Wakati wa kuokoka ndio sasa,
*Wakati wa kuliombea taifa letu kwa mzigo ndio sasa,hakuna kulaza damu!
Hapa ni kazi ya Mungu tu ,mtindo mmoja.

UBARIKIWE.


by  Gasper Madumla

Comments