Ushuhuda: Ajenga nyumba kubwa baada ya maombi.


Anastella Joseph akishuhudia muujiza wake, kanisani Efatha mwenge
SHUHUDA SHUHUDA SHUHUDA.

1. ANASTELLA JOSEPH; Aliamua kutoka mbele ya Wana wa MUNGU ili aje kushuhudia Matendo Makuu ya MUNGU wetu MKUU na Kushukuru, Anasema “Yeye alikuwa anataka kujenga nyumba ya kawaida lakini sikumoja alikwenda nyumbani kwa mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, alipomuona Mtumishi wa MUNGU jinsi alivyojenga nyumba yake nzuri alisema moyoni mwake kumbe inawezekana, aliporudi nyumbani akamwambia mume wake wajenge nyumba nzuri na kubwa kama ya Mtumishi wa MUNGU. Mume wake alisema kuwa kujenga nyumba ya kama ya Mtumishi wa MUNGU tunaweza tusiimalize lakini mke wake akamwambia kwa msaada wa MUNGU TUTAMALIZA, ndipo wakachukuwa hatua ya kuanza ujenzi na alikwenda kwenye kusanyiko Mwaka 2013 Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii alisema wale ambao wanahitaji kujenga nyumba watakapotoka KUSANYIKO hili waende kwenye viwanja vyao na nyumba zao ambazo hazijaisha wakatamke “KAZI au UJENZI WALIOUANZA LAZIMA UKAKAMILIKE”, baada ya hapo yeye akamwambia MUNGU ikifika Januari nyumba iwe imekwisha na sasa ANAMSHUKURU MUNGU amemaliza nyumba nzuri kujenga kama alivyotamani ya Mtumishi wa MUNGU.


Anastella Joseph
2. Pia anamshukuru MUNGU, alipokuwa kwenye mkesha 2013 -14 Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii alisema ukitoka hapa usiende nyumbani nenda moja kwa moja Ofisini kwako Ukaombe, yeye alikwenda akafanya hivyo, badae akachukua likizo, aliporudi kazini baada ya likizo alikuta barua ya KUMPANDISHA CHEO.

3. Jambo lingine anamshukuru MUNGU, alipokuwa Kusanyiko 2013 aliomba kwa ajiri ya kijana wake awe na AKILI na MAARIFA ili AKAFANYE MAMBO MAKUBWA SHULENI, sikumoja alimtembelea mwanaye shuleni akamwambia mwanaye akianza mtihani awe anampigia simu kila siku kabla ya kuanza mitihani, Kipindi cha mitihani ya kumaliza kidato cha Nne ikaanza na mwanaye akafanya mitihani, baada ya mitihani yakumalizika wakawa WANAOMBA na matokeo ya mtoto wake ya kidato cha Nne yakawa yametoka na MWANAYE AKAWA AMEFAULU KWA KUPATA DARAJA LA KWANZA (DIVISION ONE), kila somo alilofanya hajapata chini wa wastani wa B.

Akaendelea kusema mama huyu “SIRI YA KUFIKIA MAFANIKIO HAYA NI Kujifunganisha na Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira”, na aliendelea kusema kuwa alikuwa “MWAMINIFU KWA FUNGU LA KUMI na UTOAJI WA MICHANGO MINGINE KWA UAMINIFU” na alizidi kuendelea kusema “WAKATI mwingine nilikuwa nikitamani hata Mtumishi akisimama atangaze michango, ili nitoe..”!. Haleluya, …. Jamani MUNGU wetu ni MZURI, YESU wetu ni MZURI, Je kuna jambo gumu lolote MUNGU wetu Hasiloliweza?, HAKUNA, Huyo NDIE MUNGU WETU, NDIE YESU WETU.

Comments