UTAJIRI MZURI NI ULE AKUPAO MUNGU TU.



Mithali 10:22 Biblia inasema "Baraka za BWANA hutajirisha, wala hachanganyi huzuni nayo."

Matajiri wengi ambao utajiri wao hautokani na MUNGU huishi kwa mateso makubwa licha ya kuwa na utajiri, nimewahi kumwona tajiri 1 ambae masharti ya mganga wake(shetani)  yalikuwa  asioge siku zote za maisha yake, akioga tu mali zote zinayeyuka. 


Ndugu ni heri kung'ang'ania kwa YESU.

Nimewahi kumwona tajri mmoja ambaye haruhusiwi jua kuchomoza akiwa nyumbani, hayo yote ni masharti ya matajiri ambao utajiri wao huletwa kwao na shetani.

Nikiwa wilaya fulani huko visiwani ndipo nilipochoka kabisa , maana siku moja tulikuwa tunashuhudia ili watu wampe BWANA YESU maisha yao, lakini katika nyumba 5 za ghorofa ambazo tulitembelea kila nyumba tulikuta zezeta mmoja, kitendo hicho kilisababisha niulize kwa mchungaji wangu na wale wengine ambao tuliokuwa nao , nikaambiwa kwa maeneo hayo ili uwe tajiri lazima umtoe kafara mmoja kati ya watu wako muhimu , yaani mtoto wako au hata mzazi na kwa sababu kila mtu huko kisiwani ana wake zaidi ya mmoja, kila nyumba ambazo tulikuta mazezeta waliochafuka na kutoka udenda na kamasi wengi ni wanawake. Hiyo ni kwasababu mwanamke huko hana dhamani, na ukiwa nao wake 3 ndio kabisa ni rahisi sana kumtoa kafara mmoja ili uwe tajiri.

Ndugu zangu kwa kusudi hili BWANA YESU alidhihilishwa ili azivunje kazi zote za shetani( 1Yohana 3:8b)


Na leo katika kutafakari juu ya watu kutafuta utajiri kwa shetani , nikakumbuka andiko hilo hapo juu ambalo linasema kwamba Baraka za MUNGU hutajirisha na wala MUNGU yeye hakuchanganyii na huzuni kama ambavyo shetani hufanya.

Ndugu yangu unayesoma ujumbe huu mimi nakuomba ng'ang'ania kwa YESU ili ukae salama , ili upate utajiri halali.

Na wewe ambaye kwa bahati mbaya ulijiungamanisha na shetani ili kupata utajiri, nakuomba kwa ghafla kimbilia kanisani ili usalimishe maisha yako, maana shetani lengo lake ni kukuangamiza.

BWANA YESU leo anasema ''Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.'' -Mathayo 11:28.

Wakati wa kuokoka ni sasa.
Wakati wa kuhitaji baraka za BWANA MUNGU ni sasa.
Wakati wa WOKOVU ni sasa.
Wakati wa kumpokea BWANA YESU ni leo.

                        MUNGU akubariki sana .

                        By Peter Michael Mabula.

                       Maisha ya ushindi Ministry.

Comments