VHM WAVAMIWA NA KUIBIWA WAKIWA NJIANI KUELEKEA KWENYE HUDUMA MKOANI MOROGORO



Kundi la wainjilisti ama makomandoo wa Yesu kutoka huduma ya sauti ya matumaini au The Voice of Hope ministries iliyochini ya mchungaji Peter Mitimingi, wamevamiwa na watu wasiojulikana na kuporwa pesa zote walizokuwa nazo pamoja na vifaa vingine vya kazi wakati kundi hilo likiwa njiani kuelekea Matombo mkoani Morogoro kwaajili ya huduma.

Ambapo kwa mujibu wa mchungaji Mitimingi anasema pesa zilizoporwa pamoja zilikuwa zimehifadhiwa na mweka hazina wa safari hiyo ambaye alijeruhiwa kwa kupasuka kidogo kichwani baada ya kupigwa na chupa ya bia wakati alipojaribu kuleta ubishi wa kutoa pesa kwa watu hao. Kwa mujibu wa mchungaji Mitimingi anasema timu imekwama kuendelea na safari 'tunasubiria neema ye Bwana waendelee na safari ya huko Matombo' amesema mchungaji Mitimingi.

Kuwasiliana na timu ya VHM piga namba hii kwa maswali au kuchangia huduma yao ambayo imefanyika baraka kwa maelfu nchini kwasasa. kwa walionje ya Tanzania anza na +255 713183939 na kwa walio Tanzania piga 0713 183939.

Comments