AINA 12 ZA WATU WASUMBUFU KATIKA JAMII( 3)

Na Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministries (VHM).

AINA YA TATU
BEGA BARIDI

1. Bega ndicho kiungo chenye uwezo mkubwa wa kubeba mzigo mzito kabisa kuliko kiungo kingine chochote katika mwili.
2. Gunia zito la kilo zaidi ya 100 hubebwa sio kichwani wala kwingine bali ni Mabegani.

3. Bega Baridi ni aina ya mtu mvivu asiyetaka kufanya kazi kwa bidii.

4. Bega baridi ni mtu anayejilegeza na kukwepa majukumu yake muhimu.

5. Bega baridi anapenda sana kula tena kula vinono, lakini hataki kufanya kazi kwa mikono yake.

6. Bega baridi hutumia nguvu na jasho la wengine kujishibisha na kunufaika.

7. Mwanaume ambaye ni bega baridi humwachia mkewe jukumu la kutafuta pesa za chakula na mahitaji ya familia, ada za watoto mavazi nk na yeye huachelewa kuamka na kupitiliza mezani kunywa breakfast na kwenda kupiga “misele” au kushinda akiangalia TV huku mkewe akihangaika na vibiashara huko na huko.

8. Bega baridi amejawa na roho ya uvivu na uzembe, bila ya kuhimizwa na kufuatiliwa huwezi kufanya kazi wala hawezi kumaliza kazi aliyopewa..

Mithali 14:23
“Katika kila kazi mna faida, bali maneno ya midomo huleta hasara tu.”
2Thes 3:10
“Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu, tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi asile chakula.”
Mithali 19:15
Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa.

9. Mtu huyu hujitenga na kukwepa kuchangamana na watu.
Mithali 13:4
Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu; Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.

10. Bega baridi ni mtu anaye wahi kulala na kuwa wa mwisho kuamka.

Mithali 12:27
Mtu mvivu hapiki mawindo yake; Bali mwenye bidii anazo mali za thamani.

11. Bega baridi Hapendi kubeba jukumu lolote. Kila jukumu atakalopewa atatoa sababu au udhuru.
Mithali 20:4
Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi; Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu.

12. Yeye hupenda kupewa uhuru wa kujifanyia kile anachotaka yeye, na anapowewa huo uhuru huwa anashindwa kuutumia vizuri.
Mithali 21:25
Matakwa yake mtu mvivu humfisha, Kwa maana mikono yake hukataa kufanya kazi.

13. Bega Baridi Hapendi mambo ya kusimamiwa, na anapoachwa pekeyake hawezi kujidhibiti.

JITATHIMINI JE WEWE NI BEGA BARIDI AU UPO KWENYE MAKUNDI HAYO 9 YALIYOBAKIA? KAMA UMEBARIKIWA SEMA amen! Wengine huwa hamsemi mnasoma tu na kumezea sasa Type Amen!
Stay Tuned!

Comments