AINA 12 ZA WATU WASUMBUFU KATIKA JAMII(2)

Na Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministries (VHM).


AINA YA PILI
MKUSANYA TAKATAKA (Mama PekuPeku) GABAGE COLLECTOR

1. Mtu huyu hujiweka katikati ya watu wasio sahihi na wenye hali za moyo zilizoharibika.

2. Mtu huyu ni kama nyoka, mnyama mwenye sumu kali sana ambapo akikugonga sumu yake huweza kuenea kwa kasi sana katika mwili wa mwanadamu na kwa haraka.

3. Mkusanya takataka ni mtu mzushi na muongo anayependa kusambaza uongo na uzushi. Mambo asiyoyajua yalikotoka wala yanakokwenda.

Zaburi 52:3
Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli.

4. Kipaumbele chake cha kwanza ni kusengenya na kutapanya uongo na uzushi wenye sumu kali ya kuangamiza na kugombanisha watu.

5. Mara kwa mara hutumia muda mwingi kuzunguka zunguka kutafutiza maneno ya uzushi,uongo na umbea na kuchonganisha watu.

Mithali 14:5
Shahidi mwaminifu hatasema uongo; Bali shahidi wa uongo, pumzi zake ni uongo.

6. Mbeba takataka (mama pekupeku)Hata Pumzi yake akipumua imejaa Uwongo Mtupu.

7. Siku zote huyasema madhaifu na mapungufu ya wengine, kamwe hawezi kuyasema yale yanayo muhusu yeye.

8. Hupata nguvu ya kuzungumza na kuyasema hayo maneno ya wengine wakati ambapo mhusika anapokuwa hayupo. Mara mhusika akiingia kwa bahati mbaya, basi maelezo yake huishia hapo hapo au hubadilisha mada kwa ghafla na kujichekesha chekesha kwa muhusika aliyekuwa anamsengenya.

9. Ni kama chura ambaye yupo majini hulia na kupiga kelele nyingi lakini ukitupia jiwe moja tu, ananyamaza kimya kama vile hakuna kelele. Ndivyo alivyo huyu mama peku peku.

10. Hawezi kujisikia raha wala amani kama hajaongea uongo au mambo ya uzushi. Kuzusha na kuongea maneno ya uongo kwake ndio burudani. Kama hakuna hayo maneno yupo tayari hata kutembea umbali mrefu kwenda kukusanya na kutafutiza umbea ili aweze kuusambaza.

JITATHIMINI JE WEWE NI MKUSANYA TAKATAKA (MAMA PEKUPEKU) AU UPO KWENYE MAKUNDI HAYO 10 YALIYOBAKIA? KAMA UMEBARIKIWA SEMA amen!
Stay Tuned!

Comments