BILA KUFUATA KANUNI ZA MUNGU ZA BARAKA , HUWEZI KUPOKEA

BWANA YESU asifiwe ndugu zangu.

 Karibu tujifunze ujumbe huu ambao MUNGU amenipa. kuhusu kanuni ya MUNGU kutubariki.

 2 Nyakati 7:14-15{ikiwa Watu Wangu Walioitwa Kwa Jina Langu, Watajinyenyekesha, Na Kuomba, Na kunitafuta Uso, Nakuziacha Njia Zao Mbaya; basi, Nitasikia Toka Mbinguni, Na Kuwasamehe Dhambi Yao. Sasa Macho Yangu Yatafumbuka, Masikio Yangu Yatasikiliza Maombi Ya Watu Waomba Mahali Hapa,}. 

Ndugu Zangu MUNGU ana utaratibu mzuri sana kwetu, na ni jukumu letu ni kufuata maagizo yake.
 Hapo juu tunaona mambo 5 muhimu.

 1.   WATU WALIOITWA KWA JINA LA MUNGU{Watakao mpokea YESU}
-Walioitwa kwa jina lake MUNGU ni watu wale waliofanyika watoto wa MUNGU kupitia BWANA YESU Yohana 1:12-13 (Bali wote waliompokea(YESU)  aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU. )
-Walioitwa kwa jina la MUNGU ni watu wale wanaompenda MUNGU na kwao MUNGU ni namba moja.

2.    WATU HAO WATANYENYEKEA. 
-Kunyenyekea ni kumtii MUNGU kwa kila jambo mfano kutoa ZAKA na SADAKA. kuwa na upendo kwa watu wengine. kutokupendelea watu, kukataa uovu wote, kumkiri BWANA YESU popote walipo. N.K

3.    WATU HAO WATAOMBA.
-Hata kama watu hao watakuwa na sifa zote hapo juu lakini ni wajibu wao kuomba .
-Maombi ni mkono mrefu wa kupokea kutoka kwa MUNGU.
-Maombi ya kweli ni yale ambayo lazima yaambatane na imani.
-Maombi huboresha uhusiano wetu na MUNGU BABA yetu.
-Kama sio mwombaji uhusiano wako na MUNGU utakuwa mashakani tu maana MUNGU anaongea na wewe kwa njia ya neno lake na wewe unatakiwa kuongea nae kwa maombi hapo ndipo uhusiano utakuwa mzuri.

 4.   WATAUTAFUTA USO WA MUNGU{Kwa maombi ya kufunga au maombi mengine yeyote yaliyo sawasawa na mapenzi ya MUNGU.
-Tunajifunza watumishi wengi wa MUNGU waliutafuta uso wa MUNGU kwa kufunga mfano Ezra na wenzake waliutafuta uso wa MUNGU kwa maombi ya kufunga, Danieli aliutafuta uso wa BWANA kwa kufunga siku 21.

5.   WATU HAO WATACHA NJIA MBAYA ZOTE. 
-Njia mbaya ni kila jambo la kishetani.
-Njia mbaya ni kumsikiliza shetani na wanadamu badala ya kumsikiliza MUNGU aliye hai.
-Njia mbaya ni kila aina ya dhambi.
-Njia mbaya ni matendo ya mwili.
-njia mbaya ni kila jambo ambalo liko kinyume na atakavyo MUNGU.
 
 Wanadamu wakizingatia hayo MUNGU atawakubali na watapokea baraka zake. 

Ndugu yangu  jambo la muhimu ni kujua 

MUNGU anataka nini 
na MUNGU hataki nini 

Kama tukizingatia haya hakika  tutapokea ushindi mkuu. Ndugu zingatia kanuni hii ya MUNGU kama neno lake lisemavyo, utapokea baraka kuu. 

Wakati mwingi tunahitaji mambo mengi na tunaomba lakini majibu yanakuwa ni hafifu. Hiyo ni kwasababu hatufuati kanuni ya MUNGU ya kutubariki.

Ndugu nakuomba ufuate kanuni ya MUNGU ili upokee baraka zako.
  Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292

                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments