DIRII YA HAKI NI MUHIMU SANA KWA KILA MTEULE WA KRISTO.





BWANA YESU asifiwe ndugu yangu mpendwa.

Karibu tujifunze ujumbe huu ambao MUNGU amenipa kwa ajili yangu na kwa ajili yako pia.


Dirii ni kifaa cha  cha kujikinga ili kuzuia risasi au mishale ya adui kukudhuru.


Dirii huvaliwa kifuani pote ambapo ni rahisi zaidi kumuua mtu, Moyo pia hukaa kifuani na MUNGU anatuambia tulinde moyo kuliko yote tuyalindayo. Hapo umeona umuhimu wa moyo na umeona umuhimu wa dirii. 


Dirii ni kuzuia silaha za adui.

Dirii ya haki ni silaha za MUNGU Waefeso 6:11(Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. )

Ndugu yangu usivae dirii tu ya kawaida bali vaa dirii ya haki.


Silaha za MUNGU wakati mwingine inaitwa dirii ili kuweza kuzuia silaha zote za shetani zisitudhuru.

Tunayo mashambulizi mengi ya yule shetani lakini kwa kuwa kwetu na silaha za MUNGU au dirii ya haki, shetani hatafanikiwa.

Waefeso 6:14( Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, )



-Watu wamepoteza dirii zao na sasa wanatumia akili zao, ujanja wao na mbinu za kipepo.

-Anania na Safira walishindwa kutumia dirii kutumia dirii ya haki ila wakatumia ujanja wao wenyewe, lakini wakakosa sana na kuharibikiwa.

           KUNA MAWAZO YA HAKI YA AINA 2 KATIKA AGANO JIPYA.




1. KUSIMAMA KWA UADIRIFU.

-Kusimama kwa uadirifu ni kuhesabiwa haki mbele za MUNGU Yakobo 2:23( Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu).

-MUNGU anatutazama  sisi wanadamu ndani ya YESU KRISTO, zaidi ya hapo hawezi kukuona kwa habari ya kukupatia haki, haki ya uzima wa milele au haki yaw ewe ili adui asikudhuru maana anapomtazama YESU basin a wewe anakuona uko ndani ya YESU.

-MUNGU anatuona sisi ndani ya Mwana wake maana Mwana alitwaa dhambi zetu zote pale tulipomkiri yeye kuwa BWANA na MWOKOZI wa maisha yetu.




·      2.   TABIA NJEMA.

                              Tumerithishwa tabia njema na MUNGU.

 -MUNGU ameweka asili ya haki yake ndani yetu kwa uwezo wa ROHO wake MTAKATIFU, hivyo MUNGU anatutaka kuishi kwa haki.



      ILI KUISHI KWA HAKI LAZIMA TUYAFANYE YAFUATAYO.

·      1. Kuwa na ni ya haki.

·      2.  Kufikiri mawazo ya haki.

·      3. Kunena maneno ya haki.







                           MUNGU ANATAA.


1. Nia safi

2. Mawazo sahihi.

3. Utiifu kwake,

4. Kusema ukweli.

5. Kuwa waaminifu.

6. Kufanya kazi yetu kana kwamba YESU ndiye mkuu wetu.

7. Kuwatumikia wengine kwa furaha na haki.



ROHO MTAKATIFU ni ufunguo wa hayo yote hapo juu.

-Ukimhudhunisha ROHO MTAKATIFU utakosa ulinzi.

-Ukikosa ROHO MTAKATIFU umeondoa ulinzi maishani mwako.

-Neno la MUNGU likae kwa wingi mioyoni mwetu.

ROHO MTAKATIFU ni MTAKATIFU, Ndugu taka utakatifu kwa kukubali kuwa na ROHO MTAKATIFU.

Ili tupokee utakatifu lazima tumpokee ROHO MTAKATIFU.

Waefeso 4:30(Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi),


Ufunuo 3:4-6( Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.  Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. ),


Waefeso 6:18 ( kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; )




 Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292

Comments