HII NI ALAMA YA MUNGU KWAMBA ULISOMA NENO LAKE.


Na Mtu wa Mungu Nabii Samson Mboya   0756 809 209
HATUA 5 ZAKUTEMBEA KATIKA NJIA YA MUNG


Utangulizi:
Maisha ya kila kiumbe yana hatua za mabadiliko japo tunaishi mazingira yanayofanana ila mahitaji yetu ni tofauti tofauti  kila kiumbe kinakusudi la kuishi katika huu ulimwengu Niwazi kuwa Kufanikiwa kwa kila jambo tunalolihitaji katika maisha  tunayoishi tunahitaji muongozo na njia ya hilo jambo   Maandiko matakatifu ananatufundisha nini juu ya hayo Kumbu kumbu la torati 28:1-9
HATUA 5ZAKUTEMBEA KATIKA NJIA YA MUNGU
v  KUSIKIA KWA BIDII SAUTI YA MUNGU
v  KUTUNZA- MAAGIZO YA MUNGU
v  KUMWAMINI -MUNGU  ANACHOKUAMBIA
v  KUTENDEA KAZI -NENO LAKE ANALOKUAGIZA
v  KUTUMAINI KWA KILA JAMBO

KUSIKIA; 

Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unijulishe njia nitakayoiendea, Kwa maana nakuinulia nafsi yangu.
Zaburi 143:8 Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi.
zaburi 51:8

Neno la Mungu linahifadhi  na kutujilisha fadhili za Mungu  na njia ya kuiendea
v  Neno la Mungu linaleta Uzima wa Milele
v  Neno la Mungu  lina fadhili
v  Neno  la Mungu lina hifadhi
v  Neno la Mungu linatujulisha njia ya kupita kuendea mafanikio yetu,
v  Neno la Mungu lina leta furaha na shangwe
v  Neno linafufua mifupa iliyopondeka kufurahi
v  Neno la Mungu ni Maji yaliyo hai
v  Neno la Mungu  ni Mungu mwenyewe anayejifunuwa kupitia Neno lake,
Madhara ya kutolisikia neno,

Kutomsikia Mungu tayari wewe unaasara kubwa ya hayo yaliyotajwa hapo juu yote isitoshe bado utabaki mkiwa maana huna msaada au mwelekeo wowote umepoteza njia,
Lakini kama hamtaki kusikia maneno haya, mimi naapa kwa nafsi yangu, asema Bwana, ya kuwa nyumba hii itakuwa ukiwa.
Yeremia 22:5
KUTUNZA MAAGIZO YA MUNGU
Kutunza maagizo yote Mungu anayokuelekeza inaongeza mahusiano na Mungu
Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.
zaburi 119:10

Maagizo Maagizo ya Bwana ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya Bwana ni safi, Huyatia macho nuru.
Zaburi 19:8 
maana yake ni maelekezo anayoyapata mtu fulani ili kufikia hatima yake
Haleluya. Heri mtu yule amchaye Bwana, Apendezwaye sana na maagizo yake.
zaburi 112:1
KUAMINI KILE ANACHOKUAMBIA MUNGU
Kinachokufanya uamini kile Mungu anakuambia  kwanza  ni njinsi gani unamwamini na kuamini kunatokana na kile ulichofundishwa kikakaa ndani yako na ni kwa wingi gani Neno la Mungu limejaa ndani yako,
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Warumi 10:17

MATOKEO YA KUTEMBEA KATIKA NJIA YA MUNGU
v 
UTATUKUZWA NA MUNGU JUU YA MATAIFA YOTE YA DUNIA
v  BARAKA ZITAKUJILIA  NA KUKUPATA HUTOZITAFUTA
v  UTABARIKIWA MJINI NA MASHAMBANI
v  UZAO WATUMBO LAKO UTABARIKIWA  NA NCHI YAKO
v  MIFUGO NA VYOMBO VYAKO HAVITAPUNGUWA KITU
v  UTABARIKIWA UINGIAPO NA UTOKAPO
v  BWANA ATAWAPIGA ADUI ZAKO MBELE YA MACHO YAKO
v  ADUI ZAKO WATAPOKUJA KWAKO KWA NJIA MMOJA WATATAWANYWA KATIKA NJIA SABA
v  MAMBO YOTE UTAKAYOTIYA MKONO YATAFANIKIWA
v  UTAKUWA TAIFA TAKATIFU LA BWANA, KAMA ALIVYOAGIZA
v   
MATOKEO HAYA YANAPATIKANA VIPI?
Siku zote matokeo mazuri yanatokana na Maandalizi Mazuri ya matokeo unayoyata
Unachokitarajia kukipata kutoka kwa Mtu ni lazima Umtumainie kuwa anaweza kukutendea lile unalolitaka

Neno la Mungu nimaagizo lakini katika ulimwengu wa kiroho ni sheria,


Mithali 3:1-10
Kanuni ndiyo hiyo haibadilishwi wala kupingwa  Duwa yangu ni maombi Mungu akuongezee na kukufunulia siri hii, ili kusikia kwako kukufikishe mahali pale unakostahili, kuamini kwako kukufanye upate hitaji la moyo wako
Kutenda kwako kukuongezee Mahusiano na Mungu Wako
Kutumaini kwako kukufanye uwe imara hata ukamilifu wa dahari kufikia kurudi kwake Yesu kristo Mwana wa Mungu aliye hai,
Mungu akubariki sana akupe kuyafahamu haya uliyojifunza leo, amina........


Mtu wa Mungu Nabii Samson Mboya

 kutana na Mtu wa Mungu  Nabii Samson  pale mkoani Geita atakuhudumia Mungu amempa Neema ya kipekee kwaajili ya maisha ya watu, unaweza ukapata masomo mbali mbali anayoyafundisha CD,DVD Piga simu utapata ukihitaji huduma ya ushahuri na maombezi piga simu hii 0756 809 209 ni bure huduma hii,

Comments