HUDUMA YA ROSE MUHANDO INAPOWACHANGANYA WASAMBAZAJI KENYA

Malkia wa muziki wa injili Afrika ya mashariki mwanadada Rose Muhando ameonekana kazi zake kupendwa sana nchini Kenya hadi kufikia kampuni za usambazaji wa muziki nchini humo zikigombea haki ya kusambaza kazi zake nchini humo.

Ambapo inadaiwa kulikuwepo na kutoelewana kwa wasambazaji wawili nchini humo ambao uhalali wa kusambaza kazi za mwimbaji huyo zilihidhinishwa na watu tofauti. Umoja Audiovisual ya nchini ambayo ina hati miliki ya kusambaza kazi za mwanamuziki huyo nchini, inadaiwa ilimpa kibali kampuni ya bwana Japheth Kissanga ya nchini Kenya kusambaza kazi za Rose.

Aidha kwa mujibu wa mtandao wa nairobinews umedai kwamba kampuni nyingine ilifunga safari kisiri mpaka nchini kuja kuonana na Rose Muhando ambaye alisaini mkataba na kampuni hiyo kusambaza kazi zake nchini Kenya na kusababisha kutoelewana kwa wasambazaji hao nchini humo ambapo hata hivyo kwa mujibu wa bwana Kassanga amesema kwasasa wanaelekea kuyamaliza matatizo yaliyojitokeza na wasambazaji wenzake nchini humo.


chanzo:RUMAFRICA

Comments