IBADA MAALUM VCCT JUMAMOSI HII


Kanisa la TAG Victory Christian Centre Tabernacle, lililo chini ya mchungaji kiongozi Dakta Huruma Nkone, limeandaa ibada maalum siku ya Jumamosi tarehe 11 mwezi Mei, ambapo mgeni mualikwa atakuwa Mwinjilisti Johannes Amritzer Evangelical Mission SOS.

Tukio hili litakuwa ni kuanzia saa moja hadi saa tatu na nusu asubuhi kwenye ibada ya kiingereza na kisha baadae saa nne asubuhi hadi saa sita na nusu mchana kwenye ibada ya Kiswahili. Karibuni bila kukosa Mbezi Beach A, VCCT.

Comments