JE NI SAHIHI KWA MKRISTO KUWA MWANAJESHI?





BWANA YESU asafiwe.
Karibu katika tafakari hii kuhusu ruhusa ya mkristo kuwa mwanajeshi.
Tunajua kuna mengi yanayozungumziwa katika jeshi mfano kuua, kuteka na kudanganya ili kulinda utaifa wenu.

Biblia inabeba habari nyingi  kuhusu kutumikia jeshi.
Bibilia hasa haitaji kama mtu anastahili kutumikia jeshi au hastahili. Kwa wakati huo huo, Wakristo wanakua na uakikisho ya kwamba kuwa mwanajeshi ni jambo ambalo limeeshimika sana katika maandiko yote najua kwamba huduma kama hiyo inaenda sambamba na mtazamo wa Bibilia.

Mfano wa kwanza wa huduma ya jeshi unapatikana katika Agano La Kale (Mwanzo 14:12-16-
Wakamtwaa Lutu, mwana wa nduguye Abramu, aliyekaa huko Sodoma, na mali yake, wakaenda zao. Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania; naye amekaa panapo mialoni ya Mamre, yule Mwamori, ndugu ya Eshkoli, na ndugu ya Aneri, na hao walikuwa wamepatana na Abramu. Abramu aliposikia ya kwamba nduguye ametekwa mateka, akawapa silaha vijana wake, waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane, akawafuata mpaka Dani.Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Dameski. Naye akarudisha mali zote, akamrudisha na Lutu nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu. ),  

wakati Lutu mpwa Ibrahamu alitekwa nyara na mfalme Kedorlaoma wa Elamu, na walioshirikiana nao.

Ibrahamu aliungana na Lutu kusaidia kwa kuwaweka pamoja wanaume 318 wa nyumba yake walijifunza vita na wakawashinda Waalamu. Hapa tunaona jeshi ambalo limejiamini na kuhusika  katika jukumu muhimu , kuokoa na kulinda wasio na hatia.

Baadaye katika historia, taifa la Israeli lilianzisha jeshi la kudumu. MUNGU alikuwa akiwapigania wao na kuwalinda watu wake  lakini na jeshi lilikuwepo na kuna wakati MUNGU alitumia jeshi dogo la Israeli kuwasambaratisha maadui wa Israeli mfano pale ambapo Yoshua alikuwa akiongoza mapigano kuwapiga waamaleki huku Musa akiinua mikono ishara ya maombi ili washinde vita.

Uanzishaji wa jeshi la muda katika Israeli ulitokea  ndio maana unaona Sauli, Daudi na Sulemani wakiwa na majeshi yao ya taifa. Sauli alikuwa wa kwanza kuanzisha jeshi la kudumu (1 Samweli 13:2, Naye Sauli alijichagulia watu elfu tatu wa Israeli; ambao katika hao, elfu mbili walikuwa pamoja na Sauli katika Mikmashi, na katika mlima wa Betheli na elfu moja pamoja na Yonathani katika Gibea ya Benyamini; nao wale watu waliosalia akawaruhusu waende kila mtu hemani kwake. ; 24:2,Ndipo Sauli akatwaa watu elfu waliochaguliwa katika Israeli wote, akaenda kumtafuta Daudi na watu wake juu ya majabali ya mbuzi-mwitu).

Alichokianzisha Sauli, Daudi aliendeleza. Akaongeza idadi ya wanajeshi, na akaleta makundi makuu kutoka sehemu zingine ambao walikuwa waaminifu kwake (2 Samweli 15:19-22) na akabadilisha uongozi wa moja kwa moja wa jeshi lake na kuwa wa ule wa amri jeshi mkuu, Yoabu. Chini ya uongozi wa Daudi, Israeli ikawa yenye sheria kali katika sera za kijeshi, ilikubali nchi kama Amoni (2 Samweli 11:1; 1 Mambo Ya Nyakati 20:1-3). Daudi alianzisha mfumo wa kubadilisha vikozi kwa makundi kumi na mawili ya wanaume 24,000 watumikia mwezi mmoja wa mwaka (1 Mambo Ya Nyakati 27). Ingawa uongozi wa Suleimani ulikuwa wa amani, naye pia alilipanua jeshi, akaongeza farasi na wapanda farasi (1 Wafalme 10:26). Jeshi lilisimama liliendela (ingawa liligawanyika kwa kugawanyika kwa ufalme baada ya kifo cha Suleimani) hadi mwaka 586 B.C., wakati Israeli (Yuda) ziliangamizwa kama taifa huru kisiasa.

Katika Agano Jipya, BWANA YESU alishangazwa na afisa wa Rumi (afisa aliyesimamia askali mia moja) alipomwendea. Jibu la afisa wa jeshi kwa YESU KRISTO lilionyesha kuwa alielewa maana ya mamlaka vile vile na Imani yake kwa YESU (Mathayo 8:5-13
Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia, akamsihi, akisema, BWANA, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.  YESU akamwambia, Nitakuja, nimponye.  Yule akida akamjibu, akasema, BWANA, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona. Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya. YESU aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli. Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni; bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Naye YESU akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile. ). YESU hakuishutumu kazi yake. 

 Wengi wa wanajeshi ambao wametajwa katika Agano Jipya wanasifiwa kuwa Wakristo, wacha MUNGU, na wanaume wenye maadili mema (Mathayo 8:5; 27:54; Mariko 15:39-45; Luka 7:2; 23:47; Matendo Ya Mitume 10:1; 21:32; 28:16).

Mahali na cheo huenda vimebadilika, lakini jeshi letu lichukuliwe kuwa la maana kama lile la Bibilia. Cheo jeshini kiheshimiwe.
Kwa mfano Paulo anamwelezea Epafrodito kama Mkristo mpendwa “askari pamoja nami” (Wafilipi 2:25 Lakini naliona imenilazimu kumtuma kwenu Epafrodito, ndugu yangu, mtenda kazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mhudumu wa mahitaji yangu. ). Bibilia pia inatumia matamshi ya jeshi kwa kuelezea kuwa wenye nguvu katika BWANA kwa kuvaa silaha zote ya MUNGU (Waefeso 6:10-20 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
11 Vaeni silaha zote za MUNGU, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za MUNGU, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la MUNGU; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili; ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena. )

ikijumlisha silaha zote za askari- dirii, ngao, na kisu.

Naam, Bibilia inazungumzia kutumikia jeshi, njia ya moja kwa moja na njia ya pempeni. Wakristo wanaume na wanawake ambao wanatumia nchi kwa maadili mema, ukakamavu, na kwa heshima wakaa kwa amani wakiwa wameakikishiwa kuwa utumishi kwa wote ambao watatekeleza imekubalika na kuheshimika na MUNGU wetu mkuu. Wale ambao kwa heshima yote wanatumikia jeshi wanastahili heshima na pongezi.

MUNGU akubariki sana
Wako Peter M Mabula.
Maisha ya ushindi Ministry.
0714252292

Comments