JINSI CHAKULA KINAVYOWEZA KUKUONDOA UFAHAMU WAKO KIROHO





Chakula ni miongoni mwa vitu vinavyofanya mtu aweze kuishi. Lakini chakula hichohicho kinaweza kukuondolea UFAHAMU na UHAI wako ndani yako na kukufanya upoteze mwelekeo kabisa katika maisha yako.

Tuone mifano ifuatayo;

1. ESAU ( Mwanzo 25;29-34 )

- Hapa tunaona jinsi ambavyo chakula cha Yakobo kinamfanya Esau auze haki yake ya UZALIWA WA KWANZA haijalishi alikuwa anaijali vipi lakini chakula kinamfanya asiwe na ufahamu wa kulinda na kuijali haki yake ya uzaliwa wa kwanza inayobeba mstakabali mzima wa yeye, familia yake na hata kizazi chake mbele yake. Ndio maana watu wengi wakialikwa kwenye sherehe hata kama kuna mambo machafu yanafanyika na uovu mwingi, miziki ya kidunia inapigwa huko lakini atakwenda kwa sababu ya chakula ( ufahamu wake umetekwa na kile chakula cha sherehe hata kumfanya auze haki yake ya kuwa mwana maombi, mhubiri, mwimbaji n.k

2. ISAKA ( Mwanzo 27:11 -27 )

- Chakula kinamfanya Isaka apumbazike na kupoteza ufahamu wa kutambua janja ya yakobo.

Anamuuliza maswali mawili;

a. Imekuwaje umepata upesi namna hii?
b. Wewe ndiwe kweli mwanangu Esau?.........sauti ni ya yakobo.

Hii yote inaonesha wazi wasiwasi wake juu ya nani aliyekuwepo pale lakini Chakula cha Yakobo kinamnyang’anya ufahamu na kumfanya asiyajali hayo na hatimaye afanye makosa ya kuachilia Baraka kwa mtu asiyekusudiwa. Chakula kinaweza kukufanya ukakosa hata ufahamu mzuri wa kuomba wakati mwingine. Hii inanifanya mara nyingi niwe nakula mara mbili tu kwa siku ili nitiwe ufahamu mpya wa maombi. Na hii ndiyo maana ya Mungu kusema tufunge. Maana unapata ufahamu mpya wa utatuzi wa jjambo unaloliombea na uu ya jinsi gani uliombee. Mathayo 17;21
Yesu anafunga siku 40 ili kutafuta ufahamu wa kutosha juu ya utumishi unaomkabili mbele yake kwa miaka mitatu lakini tunaona shetani anataka kumjaribu kwa kumwambia abadili jiwe liwe mkate ( CHAKULA ) ili ampoteze ufahamu wake hatimaye aweze kukubali atakayo mwambia ( k.m kujirusha kutoka juu ya kinara, kumwabudu ili ampe ulimwengu wote n.k) yatakayo mfanya abadili mwelekeo wa utumishi wake ulliomfanya aje duniani. Mathayo 4;1-11.

Ndiyo maana Mungu akitaka akushirikishe MAMBO MAZITO YA KUFANYA lazima akujulishe USILE CHAKULA kwa muda kadhaa ili ufahamu wako uendanee na wa kwake ndipo utaweza kueelewa maelekezo na jinsi ya kulifanya jambo hilo.

Musa anafunga kwa siku 40 ni kwa sababu anakwenda kupokea MAMBO MAZITO (AMRI KUMI ) kwa Mungu mlimani yatakayokuwa msingi na maelekezo makuu kwa kizazi cha Musa na vingine vijavyo milele yote. Hii inahitaji UFAHAMU MKUBWA wa kuyapokea na kuyatoa kwa watu wale. Fahamu kuwa umesimama si kwa ajili yako tu bali ni kwa niaba ya wewe, familia yako na hata vizazi vingi mbele yako. Isaya 58;12

3. DANIELI ( 1;8 – 21 )

- Danieli kwa kukwepa chakula cha mfalme anapata ufahamu na hekima kuliko vijana wote wa BABELI. Kumbuka kina Danieli wapo pale ili kutetea kizazi na taifa la Israeli, ndiyo maana hawafanyi masihara. WAKATI MWINGINE unashuhudiwa kuacha chakula ili kuombea familia yako lakini unanyang’anywa ufahamu na kuanza kuwaza mbona mimi sina matatizo sana basi kwa ajili ya familia mimi nitaomba hivi hivi bila kufunga. Mwishowe matatizo yanapokuja kwenye familia yanakukuta wewe, watoto wako, kizazi cha tatu hata cha nne.

- Danieli anapofunga siku 21 si kwa sababu yake tu ila anasimama kama wakili wa taifa zima na kizazi kijacho cha wana wa Israeli. Eti kwa sababu mtoto wa nduguyo ndiye anayeumwa basi haufungi wakati wa kwako akiumwa unafunga. Ni ngumu sana kumwona Mungu hapo. ( Mkumbuke Ayubu 42;10 ). Danieli kwa sababu ya kuacha chakula kwa kufunga mara kwa mara anakuwa na ufahamu na uchunguzi na kujua kuwa wakati wa Yerusalemu kuwa ukiwa ( wao kubaki utumwani) umeisha. Danieli 9;1-6, 10;3. Ni wakati gani umekuwa na ufahamu ukawez kuomba na kuchimbua siri za ukoo wako ,kabila lako, taifa lako au familia yako?

4. SAULI (Matendo 9;1 – 9)

- Mungu kwa kuona umuhimu wa Sauli kuwa na UFAHAMU ili ajue ni nini anatakiwa akifanye baada ya kuongoka kwake, anampa kutokula wala kunywa kwa siku tatu mchana na usiku. Haikuwa mpango wa Sauli kutokula na kunywa , Mungu anamlazimisha kufanya hivyo kwa sababu la sivyo Sauli kabla ya kufika kwa Anania akaombewa anaweza kupotezwa ufahamu aliotiwa kwa NURU ya Yesu na kinyume chake akaanza kufikiri kurudi nyuma tena.

- Kipo chakula kimoja tu ambacho kinadumumilele na ndicho ambacho unao ulazima wa kukila siku zote la sivyo uhai wako unakuwa na mashaka. CHAKULA HICHO NI NENO LA MUNGU.

i. Ndilo ambalo lilimfanya Petro apate samaki kwa wingi mbali na kuhangaika na kukesha usiku kucha bila ya kupata kitu. Alipo kula tu hilo anasema ‘’………kwa NENO lako nitashusha nyavu’’. Luka 5; 5 – 6.

Yesu anasema, ‘’Mimi ni chakula cha uzima kilichoshuka kutoka Mbinguni, ………Baba zenu walikula mana wakafa, lakini mtu akila chakula hiki hatakufa ‘’. Yohana 6;34 – 35, 48 -51.

ii. Ni silaha kubwa katika vita na adui shetani. Ebrania 4; 12 , Efeso 6 ;11,17. Hushindi vita usipokuwa na NENO LA MUNGU ndani yako. Kama unabisha muuliza Yesu asingekuwa na Neno la Mungu ndani yake mambo yangekwendaje?. Mathayo 4 ;1 – 11, anapo sema IMEANDIKWA maana yake AMESOMA. Kumbuka shetani anayafahamu maandiko hivyo shida yake siyo kwamba UNAFUNGA tu ila shida yake ni pale unaposoma neon la Mungu mara kwa mara na kulitafakari hapo atahitaji mpaka machela kabisa imbibe huku katundikiwa dripu za maji. Hii ni kwa sababu pigo ambalo utakuwa umeachilia ni kubwa kwake, kwa kazi yake na malengo yake kiujumla.

JIULIZA NI KWANINI MWILI AMBAO UNAKUFA BAADA YA MUDA MFUPI MBELE YAKO NA KUHARIBIKA UNAUPA CHAKULA HATA MARA NNE KWA SIKU NA ROHO YAKO ITAKAYO ISHI MILELE AIDHA PARADISO AU JEHANAMU UNAINYIMA CHAKULA ( NENO ), UNAIPA MARA MOJA KWA SIKU AU HATA MARA MOA KWA WIKI, HIVI KUNA USALAMA KWELI?????

Watu wengine akiamka tu asubuhi anapiga chai nzito,ametembea tembea kakuta karanga, muhindi n.k anavipiga. Hapo bado hajakaribishwa na rafiki yake kuwa “unatumia soda gani??” Wakati mwingine kashawishiwa hata kuulizwa, “ Je, nikupe Safari lager au Kilimanjaro?”. Matokeo yake unanyang’anywa ufahamu unaanza kutokana na kufanya mambo ya ajabu ajabu hata kujidhalilisha mwenyewe. Hapo bado haujapiga mlo wa jioni na usiku. Wakati biblia kufungua na kuisoma ni mchakato mzito kwako. Saa nyingine ukiambiwa kanisani fungua wakorintho wa kwanza wewe unahangaika na Agano la kale, au la sivyo uhangaike kwanza na “YALIYOMO” utafute niukurasa wa ngapi. NI AIBU sana kwako kama MKRISTO . Chakula chako kikuu kiwe ni NENO LA MUNGU. Hicho cha mwilini ni cha ziada tu. Yohana 4; 31 – 38

Mtu anaona ni afadhali akae na kusikiliza nyimbo za wapumbavu wa Dunia ( Mhubiri 7;5) kuliko kusikiliza mahubiri ya watumishi mbalimbali au kusoma masomo mbalimbali. Waimbai wenyewe wamevaa nusu uchi, suruali zinadondoka kama vile wameishiwa fedha ya kununulia mkanda, nguo za ndani zinaonekana waziwazi na wengine wanathubutu hata kuvua nguo wakiwa majukwaani. Halafu bado unnawaita waelimisha jamii. Chakula chao wanachoachilia kimekuteka ufahamu hilo halina ubishi. Ukitaka kuamini angalia page watu wana like kwenye mitandao ya kiamii, au angalia kauli za watu wengi mitaani ameokoka lakini utasikia “hakunaga” au “mzuka umenipanda” . Ama kweli wahitaji maombi mazito wewe, ufunguliwe. Umekula chakula kichafu na kimechafua tumbo lako la ufahamu unatema na kutapika uchafu kkwa watu. Mungu akukomboe. Kwa watumishi ujue si kila mtu anaye like post yako au somo ulilo tuma kalisoma, wengine wanatoa faraja tu ujue kuwa upo nao, kumbe mioyo yao ipo mbali na wewe. Mungu saidia kanisa lako lisinyang’anywe UFAHAMU.

NIKUTAKIE TAFAKARI NJEMA YA SOMO HILI NA MUNGU AKUBARIKI!!!!!!!!!!

LIMEANDALIWA NA;

Mwalimu Nickson Kipangula – HUDUMA YA MAOMBI YA UREJESHO (R.P.S)

Email ; kipangulanickson@yahoo.com
Simu ; 0757350527

Comments