JINSI UNAVYOWAONA WATU WENGINE NDIVYO ULIVYO WEWE

Na Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministries (VHM).

Mambo 3 ya Msingi Kuhusu Mtazamo wako Kwa Wengine.

1. Matazamo Juu ya Watu
Kila mtu ni lazima waelewe kwamba mtazamo wako juu ya watu wengine unategemea sana wewe wenyewe ulivyo, Kuliko kigezo kingine chochote. Mawazo uyonayo juu ya watu wengine yanaathiri vile watakavyotuchukulia na vile uhusiano wako na wao utakavyokuwa.

2. Picha ya Msafiri Mwenye Mtazamo Hasi. (Negative)
Msafiri mmoja alipoukaribia mji fulani, alimuuliza mzee mmoja aliyekuwa ameketi kando ya njia, “eti mzee, watu wa mji huu wakoje?” Yule mzee akajibu kwa kumuuliza Yule msafiri, “Walikuwaje katika mji uliotoka?” Yule msafiri akajibu“ Aah! Hawafai, sio watu wazuri, ni watu hovyo sana, ni wakatili, wasioaminika na wenye matatizo ya kwa kila hali.” Yule mzee akatabasamu tu na kusema, “Ahah! utawaona hivyo hivyo katika mji ulio mbele yako.”

3. Picha ya Msafiri Mwenye Mtazamo Chanya. (Positive)
Mara baadaye, msafiri mwingine alisimama pale pale kwa mzee Yule na kuulizia kuhusu watu wa mji ule. Tena yule mzee alimuuliza Yule msafiri kuhusu watu wa mji aliotokea. “Msafiri akajibu. Walikuwa wa kweli, waungwana, wazalishaji na wenye moyo wa upendo na urafiki na ushirikiano.” jibu likaja. Yule mzee akajibu, “Ahah! utawaona hivyo hivyo katika mji ulio mbele yako.”

Yule mzee alikuwa na hekima sana. Alijua kwamba vile watu wanavyowaona watu wengine huakisi (Reflect) jinsi walivyo wao wenyewe.

Unaweza ukawaona watu wanamatatizo hawaeleweki eleweki, kumbe hayo unayoyaona nikivuli cha mambo uliyonayo mwenyewe.
JITATHIMINI NA KUJICHUNGUZA KWANZA WEWE MWENYEWE KABLA HUJARUSHA MAWE KWA WENGINE.

Luka 6:42 Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako.

Comments