JINSI YA KUDAI HAKI YAKO MBELE ZA MUNGU.



 
BWANA YESU asifiwe ndugu  yangu.

Nakukaribisha tujifunze jinsi ya kudai haki zetu mbele za MUNGU.

Tunajua tunadai haki kwa nani?

Haki zetu tunazidai pale ambapo tunauhitaji wa jambo Fulani mbele za MUNGU.

Ni lazima tumjue vyema tunayemdai.

Je tunasifa za kudai hicho tunachotaka?

Isaya 54:17 (Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA. )

Watu wengi hatujui jinsi ya kudai haki zetu mbele za MUNGU, Watu wengi hatufahamu tudai nini, Watu wengi hua tunajaribu tu kudai lakini hatuna imani ya kupokea na wengine hatujampokea BWANA YESU ambaye ndio chanzo cha haki yetu yote hivyo hatuwezi kupokea.


Kuna haki zinafahamika zinafahamika na kuna haki hatuzijui.

Muda mwingi unawaza ‘’hivi MUNGU hanioni?’’

Wakati mwingine unawaza ‘’Mbona Fulani kafanikiwa?’’

Yeremia 1:19 ( Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe. )

Tatizo sio kujua ila tatizo ni kutambua haki yako mbele za MUNGU.

Tujikubali kwa maneno na kwa matendo pia.

Haki ya MUNGU haionekani kwa macho hadi pale haki yako itakapofanya kazi ndio utaona matokeo mazuri.


Kutoka 15:1-18(Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini. BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni MUNGU wangu, nami nitamsifu; Ni MUNGU wa baba yangu, nami nitamtukuza. BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake. Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini, Maakida yake wateule wamezama katika bahari ya Shamu.  Vilindi vimewafunikiza, Walizama vilindini kama jiwe. BWANA, mkono wako wa kuume umepata fahari ya uwezo, BWANA, mkono wako wa kuume wawaseta-seta adui.  Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokuondokea, Wapeleka hasira yako, nayo huwateketeza kama mabua makavu.  Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa, Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu, Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari. Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara, Nafsi yangu itashibishwa na wao; Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza. Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza; Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu. Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu? Ulinyosha mkono wako wa kuume, Nchi ikawameza. Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa, Kwa uweza wako uliwaelekeza hata makao yako matakatifu. Kabila za watu wamesikia, wanatetemeka, Wakaao Ufilisti utungu umewashika. Ndipo majumbe wa Edomu wakashangaa, Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka. Hofu na woga umewaangukia; Kwa uweza wa mkono wako wanakaa kimya kama jiwe; Hata watakapovuka watu wako, Ee BWANA, Hata watakapovuka watu wako uliowanunua. Utawaingiza, na kuwapanda katika mlima wa urithi wako, Mahali pale ulipojifanyia, Ee BWANA, ili upakae, Pale patakatifu ulipopaweka imara, BWANA, kwa mikono yako. BWANA atatawala milele na milele. ).

-Maandiko hapo juu yanaonyesha Musa na wana wa Israeli walitambua haki yako mbele za MUNGU .

-Hapo juu inaonyesha kwamba huwezi kumsifu mtu usiyemuona.

-Itambue haki yak oleo kwa MUNGU.

-BWANA amkekupa haki tena, unaweza kuomba  lolote kwake  ukapata.

-Usijisahau kwamba wewe ni mwenye haki, Palilia haki yako mbele za MUNGU siku zote.

BWANA YESU asifiwe.

Usikubali kulea tatizo ndani ya moyo wako.

Usilidharau tatizo lako kwamba ni dogo sana bali shughulika nalo hata kama ni dogo sana.

Ndugu yangu uliyekombolewa kwa damu ya YESU KRISTO, Baada ya kukombloewa ulitakaswa na kupewa haki ya MUNGU katika KRISTO.

Lakini wateule wengi wana UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIROHO.

-Haki yako idai huku ukiwa na sababu kabisa kwamba haki yako ni halali kwako.

-Watu wengi huona tu vinavyoonekana lakini visivyoonekana ni vibaya zaidi, visivyoonekana ni mambo mabaya unayokusudia moyoni mwako.

Isaya 43:25-26 (Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako. Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. ).

Je unaijua kesho yako katika MUNGU ikoje?

Mambo mengine tunapanga sisi lakini tambua kwamba mengine MUNGU ndiye anapanga, lakini MUNGU hakuwazii mabaya hata siku moja bali yeye anakuwazia mema tu. Yeremia 29:11( Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. ).

Palilia maisha yako ya kiroho.

Palilia safari yako ya mbinguni.

Mfuate ROHO wa MUNGU siku zote za maisha yako.

Luka 18:1(Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba MUNGU sikuzote, wala wasikate tamaa. )



 Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292

Comments