kushugulikia vifungo
Utangulizi:
Watu wengi
wamefungwa na hawajui kama
wamefungwa kwakuwa wengi wamezoea kuona
kifungo cha kimwili mtu kufungwa jele , Vifungo
vipo vifungo vingi sana ambavyo vina watesa watu bila wao kufahamu
Kusala si kigezo cha Mtu
kuwa Huru toka katika kifungo alichofungwa
unaweza ukawa unasali,unatoa mafungu ya kumi,unafunga mara kwa mara,
inawezekana hatakuhudumu unahudumu lakini ukawa bado umefungwa,
Mara nyingi kupata
urafiki au uhusiano na mtu ni rahisi
sana lakini ili uweze kuendelea uhusiano
wenu unatakiwa kuboresha mahusiano yenu, Maandiko matakatifu yanasema kuwa
mtaijuwa kweli nayo hiyo kweli itawaweka Huru, ukishawekwa huru fahamu kuwa kuna kazi ya zihada unatakiwa
kuifanya,ili usifungwe tena,
KIZUWIZI NI NINI?
Kizuwizi ni hali au nguvu
inayomzuwia Mtu katika kufanikisha jambo flani
Kwamfano,
Ø Kutoolewa
Ø Kuto
owa
Ø Kutofanikiwa
kibiashara
Ø Kutopata
kazi
Ø Kutopandishwa
nafasi nyingine kazini (cheo)
Ø Kutopendwa
Ø Kuto
sikilizwe,
Vizuwizi vipo vingi ila
hapa kuna mfano mchache
AINA ZA VIFUNGO:
VIFUNGO VYA KIMWILI
VIFUNGO VYA KI-ROHO
Vifungo vya mwili tabia
inaweza ikakufungia mambo yako mengi yasifanikiwe. Hivyo shetani anaweza
kukuacha usonge mbele na kazi ya Mungu lakini akakuzuia kupitia vifungo vya tabia
yako tabia ni kitu kidogo sana ila kinaweza kukuzuwia katika mambo makubwa
sana, kwasababu kila mtu anapozaliwa anazaliwa na zawadi aliyopewa na Mungu
yakumuwezesha yeye kuishi katika hii Dunia,
Chakwanza
Kipawa,kipaji,nyota,Bahati, kipawa kimebatiswa majina mengi sana,
Chapili Tabia hii kwa
sehemu motto anaweza akaridhi kidogo kwa wazazi sehemu nyingine kwake yeye
mwenyewe, asipokuwa makini nyingine watu wanaridhi toka kwa marafiki au duniani
kwa mazingira anayoyaishi,
KIPAWA NA TABIA YA MTU:
Kuna vitu kadhaa vya
kuangalia Kama mtu wa Mungu unayehitaji kufanikiwa, cha kwanza ni kipawa na pili ni tabia yako mtu.
Mithali 18:16 “zawadi ya mtu humpatia nafasi, humleta mbele ya watu wakuu; ”
hili neno zawadi kwenye Biblia ya kingereza linaitwa “GIFT” au kwa Kiswahili
kipawa. Sasa basi kipawa cha mtu chaweza kumfikisha mbele za watu wakubwa na
kujulikana. Mfano mtu anaweza kuwa na kipawa cha uwimbaji lakini anakaa
kijijini na umaskini, ila kile kipawa chake kikionekana kinaweza kumleta mtu
huyo mjini hii ndio maana ya sehemu ya kwanza ya andiko hilo. Kwasababu hiyo
kila mtu aliyepo duniani amepewa kipawa na Mungu ambacho kwa hicho anaweza
kufika kwenye hatua ya juu zaidi.
Mtu anaweza akawa
hajasoma lakini kwa tabia yake Njema akapewa nafasi kubwa sana katika taasisi
au kampuni, hayo tumeyeone makanisani tumeyaona,Makazini ni mifanomingine mingi
unayo wewe, Tabia yako na kipawa chako kinauwezo wakukupatanisha hata na adui
zako maana utapoinuliwa watalazimika kukujia
Tabia na kipawa kinavuta
watu na kunakupaheshima bila ya kulazimisha, watu kukuheshimu,
Duwa na Maombi yangu
kwako baada ya somo hili Maisha yako yabadilike kabisa Roho Mtakatifu akusaidie
kukumbuka ulikopotezea kipawa chako na tabia yako,
kipawa cha mtu humleta kwenye mafanikio yake, tatizo linakuja pale
mtu anapokuwa na kipawa lakini tabia yake si nzuri. Hivyo tabia ndio ambayo
inakubakiza katika sehemu uliyopo. Mtu anaweza kuwa na macho ya rohoni au upako
lakini kama tabia yake ni mbaya hakuna mtu atakayetamani kuwa karibu naye. Ili
Mungu akutumie kwa kiwango cha juu ni muhimu kuanza kwa kubadili tabia
yako huitaji kuombewa wala kuwekewa
mikono na watumishi wa Mungu wewe badilika tu,
TABIA ZA KIMUNGU NA TABIA ZA ASILI:
Biblia imeainisha tabia
za aina mbili, yaani tabia ya Kimungu na tabia ya kiasili au ya mwilini. Katika 1Wakoritho 2:14 “Basi mwanadamu wa
tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi,
wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.” 1Wakorintho 3:1 kuna tabia za rohoni na
tabia za mwilini. Hivyo anachosema Mtume Paulo ni kwamba unapoongea na watu
inabidi ujue ama mtu huyo ana tabia za rohoni au za mwilini. Mfano mtu anaweza
kuwa mwimbaji mzuri lakini ana tabia ya uongo; wewe ni shahidi mara Ngapi
unawalika Mwiimbaji au mhubiri anawahaidi kuja kabisa mnatumia gharama nyingi
kukusanya watu mwisho haonekani swali langu kwako je hiyo ni tabia Njema au
Mbaya?
Mtu mwingine anaweza kuwa na kipawa
kitakachomfanya apate mchumba; lakini kama tabia yake ni mbaya ama uongo, au
umbeya au uzinzi inaweza kumfanya kuachwa na Mchumba wake sio kwasababu
hapendwi bali kwasababu ya tabia. Tabia ya Kimungu ni tabia njema na nzuri
lakini tabia ya kibinadamu ni tabia mbaya aliyonayo mtu.
Shetani akitaka kuharibu
kipawa cha mtu anaanzia kwenye tabia yake; kwa maana hiyo tabia ya kibanadamu
au ya mwilini ndio hiyohiyo Biblia inaiita tabia ya kishetani. Ukisoma katika Yakobo 3:15 “Hekima hiyo siyo ile
ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.”
Unaona kumbe tabia mbaya ya kinadamu ndio hiyo inaitwa tabia ya kishetani. Mhubiri 10:1 “Mainzi mafu huvundisha
marhamu ya mwuza marashi; Kadhalika
upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima.” Hili ni neno la hekima la
Mfalme Suleimani kusema mainzi wanaweza kuharibu marhamu nzuri; ikimaanisha
unaweza kupata mpenyo katika maisha lakini tabia mbaya inaweza kukupeleka mbali
kabisa na upenyo wako.
Ndio maana waweza kumkuta
mtu ni mwombaji au anatenda miujiza lakini tabia yake ikawa mbaya kwasababu ya
asili. Jambo hili ndilo linalosabisha watu wengine kusema “kama ulokole ndio
huu sitaki kuokoka” kumbe mtu huyo aliwahi kumuona mtu ambaye ameokoka na
ananena au anaombea watu lakini ni mwongo au mzinzi. Katika Biblia, Samson
alikuwa mnadhiri wa Mungu na alikuwa amepakwa mafuta tangu tumboni mwa mamaye.
Japokuwa alikuwa mpakwa
mafuta lakini alikuwa na tabia mbaya ya kutaka wasichana wa kifilisti ambao
Mungu alikataza tangu mwanzo. Hii ni sawa na mtu kung’ang’ania kufungwa nira na
mtu asiyeamini.
Kwa njia hii Samson
akakutana na Delila ambaye lengo lake halikuwa upendo bali ni kumharibia kipawa
chake kwa kuijua siri yake. Vivyohivyo shetani amewaangamiza watu wa Mungu
wengi kwa kuwafanya waoe au kuolewa na watu wasiomjua Kristo na matokeo yake
kile kipawa cha Kimungu kilichokuwa ndani yao kinashindwa kuonekana tena.kimetitia
kabisa unahitaji Msaada wa ushahuri na Maombi kwa Mtu wa Mungu zamani punda akipotea watu walikimbia mbio
kwa Mtu wa Mungu kuuliza siku za leo hawana Muda kabisa wa kuwauliza watu wa
Mungu,
UFANYE NINI JUU YA HAYA? BADILISHA MWENENDO WA TABIA YAKO
LEO:
Tabia mbaya ya mtu
huondoka kwa kuamua mwenyewe, hata kama mchungaji akuombee mara zote kama tabia
yako ni mbaya kwa asili inakulazimu kuamua kuibadili mwenyewe. Ni kweli tabia
yako inaweza kuwa imeshakupotezea kibali kwa watu au imeshakupotezea upenyo
katika maisha lakini ukiamua kuanza upya na BWANA na kuacha zile tabia mbaya
Mungu wetu ni wa nafasi ya pili. Mungu wetu anatoa nafasi ya pili biblia
inasema, “usifarahi ee adui yangu niangukapo mimi nitasimama tena” mwenye haka
ananafasi saba za kuinuka ijapokuwa ataanguka, simaanishi ukajiangushe ili
uinuke mara saba hapana aliyesimama asijisifu bali angalie asije kuanguka,
Leo naongea na watu ambao
walikuwa waombaji leo hawaombi tena, walimuhofu Mungu lakini leo hawana hofu,
walikuwa watakatifu lakini leo ni waovu wakubwa Mungu anayo nafasi ya pili
kwaajili yako. Amua kutubu na kuacha dhambi na tabia hiyo mbaya; Mungu
atakuwezesha tena kama alivyomwezesha Samson kuwaangamiza wafilisti wote. Hivyo
uamuzi wa kwanza ni kuamua mwenyewe kuacha tabia hiyo.
Nimeamua kumtolea mfano
Samson maana hakuna asiyejuwa mwanzo wa Samson na mwisho wake,
Hii ndiyo nafasi yako ya
dhahabu
Kwamsaada na ushahuri
wa Maombi na Maombezi wasliana na
Mtu wa Mungu Nabii Samson
0756 809 209
Comments