KUYAPINGA MATENDO YA MWILI NA KUENENDA KATIKA ROHO.

Kuyapinga matendo ya mwili ni hali ya kukataa matendo ya mwili ambayo yanapingana na Mungu na matendo hayo ni dhambi mbele za Mungu.

 Na haya ndio matendo ya mwili:-

 UASHERATI, UZINZI,
 ULEVI, KUABUDU SANAMU, 
WIZI, ULAFI, 
UCHAFU, UFISADI, 
 UCHAWI, UADUI, 
UGOMVI, WIVU, 
HASIRA, URAFI, 
UONGO, MATUSI, 
TAMAA MBAYA, 
MAWAZO MABAYA, na mengineyo... 

Na Mtumishi wa MUNGU,Alex.
Na kuenenda katika ROHO ni kuyatenda yaliyo mapenzi ya Mungu na kazi hii inafanywa na Roho Mtakatifu ambaye humuongoza mtu kuyatenda yaliyo mapenzi ya Mungu. 

 Na haya ndiyo matendo ya roho:- 
UPENDO, AMANI, 
FURAHA, UVUMILIVU, 
UTU WEMA, FADHILI, 
UAMINIFU, UPOLE, 
KIASI, na mengineyo kama haya... 

Maandiko yafuatayo yanaonyesha na kutufundisha jinsi ya kuyapinga matendo ya mwili na kuenenda ktk roho.. 
WAGALATIA 5:16-25, WARUMI 8:5-14, WAKOLOSAI 3:5-11, WAEFESO 4:17-24, 1PETRO 2:11, WAEFESO 5:3-13.

 Hebu chukua muda kupitia haya maandiko naamini utajifunza kitu na Mungu akubariki..!!, 

BY ALEX WA JESUS.

Comments