KUZALIWA MARA YA PILI

Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania


Ni kweli kua,kila mtu alishazaliwa kwa habari ya mwili!Lakini,imempasa kila mtu kuzaliwa kwa maji na kwa roho.Kuzaliwa huku,ni kule kumpokea Yesu Kristo na kufanyika upya!Ni hatua ya muhimu sana.(Yn3:1-11)

Yesu mwenyewe anasisitiza kua,kila mtu yampasa kuzaliwa mara ya pili(Yn1:12&13)

Huku kuzaliwa kwa mara ya pili,mtu hubadirishwa,na hii si kwa mapenzi ya mtu bali ni kwa mapenzi yake mwenyezi Mungu(1Yn3:9-12,4:7)

Kuzaliwa huku,humtambulisha mtu katika ufalme wa Mungu kwa kumpokea Kristo"kila aaminiye kuwa Kristo ni Bwana,ni mwana wa Mungu"1Yn5:1)

Hili linamaanisha kwamba,ukimpokea Yesu,anakuja ndani yako,na wewe ndani yake na kufanywa upya!hivyo unakua umezaliwa na kuwa kiumbe kipya(2Kor5:17).

Mtu huyu aliezaliwa mara pili,kwakua yu ndani ya Mungu huyasitahili majaribu(Yak1:18) wala hatawaliwi na dhambi(Rum6:12).Maisha yake yamejaa upendo,furaha,amani(Gal5:22) na ushindi siku zote,huzishinda ngome za ibilisi(Gal5:19-21).Daima ni mtiifu kwa Mungu(1Sam15:22).


 Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.
Kwa Mobile +255(0)7 (57/84) 464 141/ 12 909 021.
Au Email sos.sesi@yahoo.com / newelshaddai@gmail.com

Tunakushauri, utembelee kanisa la kiroho lililo jirani yako, kwaajili ya mafundisho zaidi na Ushirika. (Kumbukumbu la Torati 28:6).

Comments