BWANA YESU
atukuzwe watu wa MUNGU.
Namshukuru
MUNGU kwa uzima aliotupa, na ushindi ambao anatupa kila siku.
Ndio maana
sisi siku zote ni washindi , na tunashinda na zaidi ya kushinda kwa YESU
aliyetupenda.
Ujumbe wa
leo unazungumzia MATOKEO YA MAOMBI YETU.
Matokeo ya
maombi yetu yanaweza kuwa ndio au hapana , yaani kupokea kile tulichoomba kwa
wakati au kuchelewa kupokea kwa wakati na wakati mwingine tukokupokea kabisa.
ZIFUATAZO NI
SABABU 11 ZA KWANINI TUNACHELEWA KUPOKEA AU HATUPOKEI KABISA KUTOKA KWA MUNGU
KWA YALE TULIYOOMBA KWAKE.
1. KUOMBA VIBAYA; Yakobo 4:3 ( Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
).
2. HATUNA BIDII YA MAOMBI; Mithali 8:17( Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.
).
3. KUTOMPENDA BWANA
YESU; Mathayo 11:28( Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
),
Yohana 14:6 (YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi.
),
Matendo 4:12( Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina
jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa
kwalo.
),
Yohana 14:14(Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.
).
BWANA YESU
asifiwe, hapa tunajifunza kwamba maombi yetu yote lazima tuombe katika jina la
YESU KRISTO, Tena tunajifunza kwamba hakuna wokovu wala hakuna kupokea uzima wa
roho na afya zetu kutoka kwingine kokote ila ni kwa BWANA YESU. Sasa kama
hatumpendi BWANA wala hatumhitaji hatuwezi kupokea chochote kutoka kwa MUNGU
hata kama tumeomba sana.
4. DHAMBI; Isaya 59:1-2(Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
).
5. TAMAA; Yakobo
5:5( Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo.
).
6. SHETANI; Daniel
10:11-13 ( kaniambia, Ee Danielii, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo,
ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno
hili, nalisimama nikitetemeka.
Ndipo akaniambia, Usiogope,
Danielii; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu,
na kujinyenyekeza mbele za MUNGU wako, maneno yako yalisikiwa; nami
nimekuja kwa ajili ya maneno yako.
Lakini mkuu wa ufalme wa
Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli,
mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko
pamoja na wafalme wa Uajemi.
)
Shetani
huzuia maombi, hivyo tunatakiwa tuitumie mamlaka ya KRISTO iliyo ndani yetu
kumwadabisha maana ni mwoga sana kama sisi tukiwa na KRISTO YESU, Hapo juu
tunaona kwamba alimzuia malaika ili majibu ya maombi ya Danieli yasifike kwa
wakati.
7. HATUOMBI; Yakobo 5:16(
Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
).
8. KUTOKUSAMEHE; Mathayo 6: 14-15( Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na BABA yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala BABA yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
).
9. MASHAKA; Yakobo 1:6-7( la na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama
wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa BWANA.
).
10.
KUKOSA
MAARIFA YA NENO LA MUNGU; Hosea 4:6a( Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa).
Mithali 1:7( Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.)
11.
HATUNA IMANI
; Yakobo 5:15( Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na BWANA atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.
)
BWANA YESU
asfiwe.
Naamini
umejifunza kitu na pia naamini umejua kikwazo chako cha kutokupokea ni nini.
Kama ni dhambi acha dhambi, kama ni kukosa maarifa ya neno anza leo kujifunza
neno la MUNGU pamoja na wenzako kanisani pia jisomee wewe mwenyewe. Kama
kikwazo chako huna YESU KRISTO basi okoka leo ili uwe na haki ya kuomba na
kupokea kutoka kwa MUNGU. Na kama kikwazo chako ni moja ya vipengele hapo juu,
tengeneza ndugu na utaanza kupokea kwa BWANA.
Kwa leo naishia hapo,
MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea
BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na
atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu
kwa mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana
makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani
aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
Comments