KWAYA YA UINJILISTI KUTOKA EAGT MIKOCHENI A WAZINDUA DVD YAKO KWA KISHINDO.

Utawapenda uinjilisti choir, hapa wanaenda kuimba baadhi ya nyimbo zao kutoka katika albamu yao iliyozinduliwa leo.
Kawa ya ya uinjilisti EAGT Mikocheni A leo wamezindua DVD yao ya albamu yao ya 4 iitwayo AWEZA KUTENDA TENA. Kwaya hii maarufu wamefanya kweli huku wakisindikiwa na kwaya mbali mbali pamoja na waimbaji binafsi. Baadhi ya kwaya zilizowasindikiza Uinjilisti Choir ni pamoja na Majestic Singers kutoka EAGT City Center kwa mchungaji Froliani Katunzi, K PC Choir kutoka Kawe kwa Mchungaji Elly Boto, Haleluya Choir kutoka Morogoro, Samaria choir, Jerusalem Choir na nyingine nyingi.
Katika uzinduzi huo zaidi ya Milioni 3 zilipatikana ambapo mgeni rasmi Eng Benjamini Mwendapole alitoa Milioni 1 na nusu . Hizi ni baadhi ya picha katika tukio hilo ambalo Maisha ya ushindi tulikuwepo na kushuhudia. Pia kama unataka DVD yajo ya albamu hii ya AWEZA KUTENDA TENA wasiliana nao kwa namba 0713504950, au 0652766281 na 0715425427

Wakati wa kusifu na kuabudu

Samaria choir walikuwepo kuwasapoti Uinjilisti Choir

Jerusalemu choir wakiwa kazini

Kutoka kushoto ni mgeni rasmi, Eng Benjamini Mwendapole, Katikati ni Mchungaji Elly Boto kutoka KPC Kawe na kulia ni Askofu Philemon Phiri ambaye pia ndio mwenyeji.

K P C Choir kama kawaida walikuwepo, Hapa wakijiandaa kuimba wimbo uitwao NIMEKOMBOLEWA KWA DAMU YA YESU.

Ni zamu ya K PC Choir kuimba

Ni live kabisa, safi sana vijana wa K P C

Haleluya choir kutoka Morogoro wakiwasha moto wa injili iliyo hai.

Kutoka Maisha ya ushindi Scholar alikuwepo.

Watu walikuwa ni wengi sana, Hapa kwaya ya uinjilisti wakiingia stejini kwenda kuonyesha kwamba wanazindua video ya nyimbo bomba sana.




Baadhi ya waliofika katika uzinduzi wa kwaya ya uinjilisti.

Huku wakishangiliwa sana , kwaya ya uinjilisti mikocheni wakiwajibika , hapa wakiimba wimbo wa mwisha katika albam yao . Wimbo unaitwa MAISHA


Askofu Philemon Phiri akipanda madhabahuni ili kuomba kwa ajili ya kuanza rasmi kwa uzinduzi.



Watoto wa Mchungaji Froliani Katunzi, Majestic Singers walikuwepo, Hapa waliimba wimbo bora uitwao MIFUPA MIKAVU.


Mgeni rasmi Eng Benjamini Mwendapole akikata utepe, na kununua DVD ya kwaya ya uinjilisti kwa Tsh. Milioni moja na laki tano.

Mgeni rasmi pamoja na wageni wengine waalikwa wakipiga picha ya pamoja na kwaya ya uinjilisti Mikocheni A. EAGT

Comments