Na Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima. Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe |
Utangulizi
Aina za laana;
·
Laana ya
wanadamu ,hii inaweza kuwa laana inayotokana na wazazi kwa mfano Nuhu
alipomlaani mjukuu wake Kaanani ,
tukajifunza kwamba anayekulaani siyo kwamba lazima akuambie nimekulaani bali anaweza akasema tutaona kama utafanikiwa hiyo ni
laana tayari .
·
Laana ya
Mungu, kwenye kitabu cha Malaki
Mungu anasema umelaaniwa kwa kumuibia Mungu sadaka zake.
·
Laana ya
uchungu , mtu anaweza kuwa na uchungu moyoni hata baadaye ukaleta laana
maishani mwake.
· Laana ya
majira ya kupanda na kuvuna, hii inatokana na matendo ya mtu anayotenda kama ni mema atapokea mema na kama ni maovu baadaye yatampata mabaya.
· Laana ya
shetani , shateni naye anaweza kumlaani mtu kupitia wakala wake mfano
wachawi.
Somo:
Laana ya wachawi (shetani)
Wachawi wanaweza kumlaani mtu na
akalaaniwa, kwa maana wanalaani kwa
kutoa kafara inayoimarisha laana hiyo. Hesabu
25:1-25 (Tunaona watu walitoa sadaka
kwa miungu), Kumbukumbu 32:17( watu walitoa sadaka kwa pepo), 1Samwel 26:19 ( walitoa kafara na ujira kwa mizimu), 1korintho 10:20( hata agano jipya
tunaona watu wanatoa kafara kwa mashetani). Kwa hiyo tunajifunza kuwa wachawi wanaweza kumlaani
mtu kwa kutoa kafara, kwa hiyo ni muhimu
sana kujua silaha zao na mbinu za
wachawi ili nasi tuweze kuwadhibiti kwa
jina Yesu, maana ndiyo wametuzunguka katika maisha yetu.
Hesabu 22:1- 25,
Tunaona Balaki Mfalme wa Moabu
anakwenda akiwa na ujira, kumkodi Balamu mganga ili aweze kuwalaani wana
wa Israel, ili atakapopigaana nao apate ushinda. Hii inatufundisha kuwa mtu
hawezi kushinda vita akiwa amelaaniwa. Lakini Balamu alipotaka kuwalaani wana
wa Israel alipanda mlimani na kuwaona vyema wana wa Israel. Hii inaonyesha kuwa
ili mtu alaani, lazima akae pembe fulani, maana siyo kila eneo unaweza kutoa
laana ikampata mtu.
Balamu alipotaka kuwalaani Israel Mungu iligeuza kinywa chake, na akaanza kuwabariki
wana wa Israel badala ya kuwalaani. Hii inatufundisha kuwa laana za wachawi
haziwezi kuwapata watu waliookoka. Kwa hiyo tunaona mtu asiyekupenda anaweza
kwenda kwa mganga na kumpa sadaka na kumwambia akulaani. Mganga baada ya
kupokea ujira/sadaka ndipo anapoanza kutuma mashetani yanayoweza kumdhoofisha
mtu rohoni na baadaye kushindwa kunatokea mwilini. Leo kwa jina la Yesu kila
mchawi anayerusha laana katika ulimwengu wa roho naamuru imrudie mwenyewe kwa
jina la Yesu.
Kwanini waganga wa kienyeji wanataka ujira wa kuku au
mbuzi ili wapate kumlaani mtu. Waganga
wanapopokea kuku au mbuzi wanachinja na kumwaga damu , na damu hii ni uhai, kwa
hiyo inapomwagwa na maneno ya laana yanatamkwa ndipo damu inayabeba hayo maneno na kuanza kuyaongea kila mara.
Kwa hiyo mashetani wanaposikia sauti ya
damu ndipo wanaanza kwenda kumfuatilia yule mtu aliyetamkiwa maneno ya laana
ili wayatimize. Kwa hiyo mahali hapa watu wengi wana matatizo mengi kwa maana
wamelaaniwa na kuna damu mahali inaendelea kutamka hiyo laana katika madhabahu
za wachawi. Usione watu wengi wamefanikiwa mwilini siyo kuwa wamefanikiwa tu
bali kuna kitu kimefanyika katika ulimwengu wa roho. Na sisi watu wa Mungu
tunakuja kanisani ili katika ulimwengu wa roho tupate kuharibu kila kazi za
ibilisi kwenye maisha yetu.
Ukiri:
Kwa jina la Yesu naiteketeza laana yoyote iliyatamkwa juu
yangu na kafara ya damu iliyomwagwa mahali popote kwa ajili yangu nainyamazisha
kwa jina la Yesu.
Imeandikwa mwana wa Adamu alidhihirishwa apate kuzivunja kazi
za ibilisi , kwa jina la yesu leo nasafiri katika ulimwengu wa Roho mahali popote
zinapotokea laana za kuwalaani watu naziharibu kabisa kwa Jina la Yesu.
Imeandikwa Roho wa Bwana yu juu yangu kwa maana amenitia mafuta kuwatangazia
wafungwa kufunguliwa kwao.
Nawatangazia watu wote
walionilaani niko huru kwa jina la Yesu
na mashetani wa laana nawateketeza kwa jina la Yesu. Kwa maana damu ya Yesu imemwagika ili
wafungwa wa rohoni wapate kuwa huru , na leo nayavunja magereza yote ya
magonjwa , laana, mikosi, kukataliwa kwa jina la Yesu.
Hapa duniani hakuna kitu kinachoweza kutokea bila kichocheo
hasa katika ulimwengu wa roho. Kwa hiyo
usidhani matatizo uliyonayo yametokea yenyewe, hapana kuna laana mahali
inayokufuatilia. Kwa mfano mtu anaweza kubaki kazini muda mrefu bila kupata
promosheni lakini akafikiri kuwa ni
kawaida siyo kawaida maana wafanyakazi wenzake wanaweza kumlaani ili abaki pale
bila kupanda cheo. Kwa jina la Yesu leo naamuru mtu yeyote aliyefanya ushirikina au kumwaga damu kwa
ajili yangu vimrudie mwenyewe kwa jina la Yesu.
Damu inapomwagwa mahali inaendelea kunena siku zote na
mashetani wanakuwa wanaitii sauti ya hiyo damu na kumfuatilia yule mtu. Kwa
hiyo ili mtu ashinde kwenye matatizo yake lazima anyamazishe ile damu ndipo
mashetani wanakosa nguvu na kumwachilia mtu.
Tunaweza kunyamazisha damu za kafara kwa damu ya Yesu kwa maana
imeandikwa nao wakamshinda kwa damu ya Mwanakondoo.
Maombi
Kwa jina la Yesu, baba leo nakata kamba zote za laana zilizo
kwenye maisha yangu. Imeandikwa nao wakamshinda kwa damu ya Mwanakandoo , kwa
damu ya Yesu nainyamazisha damu ya mabaya, mikosi, kuachwa,umasikini kwa jina
la Yesu. Imeandikwa bomoeni bomoeni hata msingini leo kwa jina la Yesu nabomoa
madhabahu zote ambapo kafara za damu zilimwagwa kwa ajili yangu kwa damu ya Yesu.
Imeandikwa twaeni upanga wa roho ambao ni neno la Mungu nami natwaa upanga
nawafyeka mashetani wote walioutumwa kutoka kwenye madhabahu za laana za wachawi kuja
kuniangamiza kwa jina la Yesu.
Ewe damu unayenena mabaya juu yangu nyamaza kwa jina la Yesu,
imeandikwa kwa maana kushindana kwetu siyo juu ya damu na nyama bali ni juu ya
falme mamlaka wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya
katika ulimwengu wa roho . kwa jina la Yesu nakwenda rohoni pande zote na mahali popote ilipotamkwa laana
juu yangu naiharibu kwa jina la Yesu.
Naweteka nyara makuhani wote wa giza na kuwachinja na madhabahu zazo zote nazibomoa kwa jina la
Yesu.
Imeandikwa je kuna shirika gani kati ya nuru na giza? Kwa
jina la Yesu kila mtu aliyepeleka jina langu kwenye madhabahu za wachawi leo
naliondoa jina langu kwa jina la Yesu. Naliondoaa jina langu kwenye madhabahu ya aibu,
madhabahu za umasikini, madhabahu za magojwa na kuliweka katika madhabahu ya Yesu Kristo ambayo ni madhabahu ya ushindi.
Najitenga na maneno yote yaliyotamkwa kwa ajili yangu kwenye madhabahu za
wachawi kwa jina la Yesu. Imeandikwa kila pando asilolipanda baba yetu wa
mbinguni litang’olewa kwa jina la Yesu nawaamuru mashetani wote waliondani
yangu kama wasimamizi wa laana kuniachia kwa jina la Yesu.
![]() |
Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe |
Comments