MAADILI MEMA YA KIJANA KATIKA USAFI MAENEO 12 YA MWILI WAKE

Na Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministries (VHM).

I. Maadili ya Usafi wa Kijana Kichwani – Nywele
• Uhakikishe nywele zako zimesafishwa na kuchanwa au kusukwa vizuri zisikae kama kipilipili au katani.

• Kama binti unasuka basi usuke ieleweke au kama hausuki basi uchane vizuri nywele za kichwani zikae katika hali ya usafi.

• Kijana kama unanyoa basi unyoe na usinyoe mitindo ya ajabu ajabu ambayo haina utukufu kwa Mungu.

• Hatumtarajii kijana mwenye maadili mema kusuka nywele kama msichana. Hayo sio maadili mema ya kijana wa kitanzania.

II. Maadili ya Usafi wa Kijana - Machoni
• Kama kijana uhakikishe unajisafisha vizuri macohoni usitembee kumbe una matongotongo machoni.

• Unaamka badala ya kwenda kujisafisha uanatafuta chai ipo wapi. Unakunywa chai hata macho hayajajua maji.

III. Maadili ya usafi wa Mdomoni
• Kwanza uwe na usafi wa maneno yanayotoka kinywani mwako yawe na usafi.

• Kuna baadhi ya vijana wakikusogelea hutaki kuwa nao karibu kwajili ya harufu mbaya inayotoka mdomoni.

• Kijana ahakikishe anapiga mswaki kila siku ikiwezekana mara mbili kwa siku na atumie dawa.

• Kijana asisukutue mdomo kwa kutumia vidole na maji tu.

IV. Maadili ya Kijana Kidevuni
• Kama ni kijana wa kiume uhakikishe unakitengeneza kidevu chako mara kwa mara usiachie mandevu yakajiotea bila ya utaratibu wowote.

• Ukiamua kufuga ndevu basi ujue na kuzihudumia sio mpaka zinasokotana na kuwa chafu mpaka zinaleta kinyaa.

• Wakati mwingine unakula vitu, juisi miwa nk matakataka yanabakia kwenye ndevu zinakuwa na kinyaa.

V. Maadili ya Usafi wa Kijana Puwani
• Uhakikishe kuwa puwa yako ipo safi mara zote kusiwepo na makamasi yanayo ganda mana puwani na kuleta kinyaa kwa wanaokutazama.

• Uwe na mazoea ya kutumia kitambaa mara kwa mara kujisafisha na kujikagua pua zako.

VI. Maadili ya Usafi wa Kijana - Nywele za Makwapani
• Kwa kawaida nywele za makwapani husababisha jasho na kuleta harufu mbaya, Kijana mwenye busara ahakikishe kwamba ananyoa nywele zote za makwapani mara kwa mara.

• Kijana asivae nguo ambazo zinaonyesha makwapa yake yakiwa ni machafu kwani huleta kinyaa kwa watu wengine.

VII. Maadili ya Usafi wa Kijana - Nywele za sehemu za siri
• Kuwepo kwa nywele za sehemu za siri wakati mwingine husababisha uchafu na harufu mbaya.

• Wapo baadhi ya vijana ambao huwa wana fuga na kuzisuka hizo nywele za sehemu za siri huo sio urembo bali ni uchafu ambao huleta harufu mbaya.

VIII. Maadili ya Kijana - Usafi wa kucha
• Kucha zikatwe mara kwa mara zikae katika hali ya usafi.
• Kwa wale wanaofuga kucha wahakikishe wanazifanyia usafi wa mara kwa mara ili zisiweze kutunza uchafu.

IX. Maadili ya Kijana - Usafi wa nguo za ndani
i. Chupi
Chupi zivaliwe mara moja tu kwa siku. Mtu asivae chupi hiyo hiyo mara ya pili bila ya kufuliwa kwanza.

ii. Sindilia, Shumizi na under sket kwa wasichana
Zinapaswa pia kuvaliwa mara moja kwa siku zisivaliwe tena mpaka zimefuliwa.

iii. Soxi
Kijana avae soxi mara moja kwa siku asirudie kuvaa soxi hizo mara ya pili kabla ya kuzifua. Pia ahakikishe kuwa soxi hizo hazijachanika au kuchakaa.
NB. Kijana avae nguo za ndani ambazo hazija chanikachanika au kuchakaa sana hii inaweza kuleta aibu sana wakati ikitokea dharura yeyote.

X. Usafi wa Wasichana (mwezini)
Ni muhimu wewe kama binti kufahamu tarehe zako za mwezi, ingawa inawezekana zikawa zikibadilika badilika mara kwa mara lakini jambo la muhimu hapa ni kujjiandaa kwa wakati wowote itakapo kutokea uwe na namna ya kujisitili. Itakuwa ni aibu sana wewe kama binti uliye okoka kuingia katika siku ukiwa katika maeneo ya mkusanyiko wa wa watu. Kama unawasiwasi na siku basi uvae kwa tahadhari kama itajitokeza.

Pia huu ni wakati ambapo msichana atahitaji kuzingatia usafi labda kuliko wakati mwingine wowote. Kama utakuwa na uwezo ni vizuri ukawa na Pad lakini kama itashindikana kuapata Pad basi uanweza kutumia vitambaa lakini uhakikishe kuwa vipo katika hali ya usafi wa hali ya juu. Usitumie vitu kama toilet paper au sponchi kwani watalaam wa afya wanasema huweza kusababisha magonjwa kwa mtumiaji.

XI. Usafi wa Nyumbani
Ni ajabu unaweza kumuona kijana au binti anaonekana safi amevaa vizuri lakini ukienda mahari anapoishi huwezi kuamini, ukiingia anapo lala utafikiri umeingia kwenye banda la mbuzi, ni kuchafu, kitanda hakijatandikwa mashuka ni machafu nk. Usafi wa nyumbani ni wa muhimu sana kwa kijana wa kikristo.

XII. Usafi baada ya kujisaidia
Kwa wasichana ni vema wakawa na kitambaa au toilet paper cha kujifutia ili kuzuia harufu mbaya ambayo inaweza kusababishwa na mabaki ya haja ndogo kama hayakufutwa vizuri
Kwa wavulana wanapaswa kuji kung'uta vizuri sehemu zao za siri mara baada ya kujisaidia ili yasiwepo mabaki ya haja dogo ambayo yanaweza kusababisha uchafu na harufu mbaya.
NB. Kuhusu haja kubwa ni vema kijana aka hakikisha kuwa vitu anavyo vitumia kujisafishia ni vizuri na kwamba vitamuacha akiwa safi baada ya kujisaidia
Usitumie vitu kama vipande vya maboxi, makaratasi magumu au
majani katika kujisafisha kwani havitaweza kumsafisha vizuri ipasavyo na kumuacha akiwa na mabaki ya uchafu hivyo itasababisha harufu mbaya kwake na kwa watu wengine pia. Wakati mwingine ianweza kukuletea maumivu wewe mwenyewe

12. Mavazi ya nje
Kijana avalie mavazi ambayo yatakuwa safi yaani yamefuliwa na kupigwa pasi. Kama ni vazi linalo hitaji kuchomekewa basi lichomekewe
Kama ni vazi linalo hitaji kuvalia tai basi uvalie n.k
Viatu pia viwe vimefuliwa vizuri au vime pigwa kiwi safi kabisa.
Hivyo ndivyo kijana wa kikristo anapaswa aweze kuwa.

Comments