MAKUNDI 4 YA WAZAZI KUHUSU NIDHAMU KWA MTOTO

Na Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministries (VHM).
Kundi - 1
Wazazi wenye HOFO KUBWA.
i. Kundi hili huogopa kutoa nidhamu watoto wao.
ii. Huogopa kwamba watoto hawatajisikia vizuri.
iii. Katika kundi hili mtoto ana nguvu kuliko wazazi.
iv. Atakacho kisema au kitaka mtoto inabidi wazazi wafuate hata kama hawapendi au hata kama wanajua kina madhara mbela ya safari
v. Mtoto hujipangia masharti na ratiba zake na na hataki mtu yeyote amuingilie.
vi. Katika utuuzima wake mtoto huyu huwa mbabe, msumbufu na mkorofi.
vii. Mahali popote atakapokuwa iwe kazini kanisani au popote huwa wawezi kuishi na watu vizuri lazima agombane na kila mtu kwasababu alikosa baadhi ya malezi muafaka kutoka kwa wazazi wake.
viii. Wazazi huishi maisha ya huzuni na maumizu moyoni kwa kushindwa kumlea mtoto wao katika nidhamu bora.

Kundi - 2
Wazazi WALIOJIWEKA MBALI.
i. Kundi hili halifanyi wajibu wao kama wazazi.
ii. Huwaachia na kuwategemea watu wengine kama wachungaji makanisani, walimu wa Sunday School makanisani na walimu wa mashuleni ndio wahusike katika kumfundisha mtoto wao nidhamu.
iii. Kama ni mama anajiweka mbali na mambo ya nidhamu kwa mtoto wake na kuacha jukumu hilo kwa baba wa mtoto. Mtoto akikosea adhabu inabidi ipelekwe mbele mpaka baba akirudi.
iv. Mtoto anajenga tabia ya kumdharamu mama au wazazi wote na kuwaheshimu wale wanaohusika zaidi na kumwadhibu.
v. Wengine wanawapenda watoto sana kiazi kwamba kumadhibu ni kuingilia ile hali ya kumpenda mtoto na kuona kwamba mtoto ataona kumbe sasa mzazi hanipendi tena.
vi. Mtoto katika utuuzima wake atakuwa hana hekima. Kiwango chake cha hekima kitakuwa chini sana na atashindwa kufanya maamuzi kwa kutumia busara na hekima.
vii. Hata kuwa na uwezo wa kujijengea nidhamu binafsi (self-discipline).

Kundi - 3
Wazazi WAKALI SIKU ZOTE
i. Watoto hujiepusha kuwa karibu na wazazi kama hawa.
ii. Mzazi akiingia nyumbani badala ya mtoto kumkimbilia kumpokea mzazi anakimbilia kujificha au kujifanya amelala usingizi mzito.
iii. Wakati mwingine huondoka nyumbani na kamwe hawataki kurudi tena nyumbani. Sio watoto wote walioko mitaani ni watoto wa mitaani wengine wana wazazi kabisa ila wamekimbia kutokana na ukali wa wazazi.
iv. Wazazi wa kundi hili wanatazizo la halizao za mioyo. Mioyo yao imekufa ganzi hawana huruma wala upendo hata kama ni watoto wao wa kuwazaa.
v. Wazazi katika kundi hili huwaazibu watoto wao kwa kutumia vitu kama:
• Kisu
• Panga
• Shoka
• Nyundo
• Mtwangio
• Chupa n.k
vi. Watoto katika kundi hili hujenga hali ya uwongo, ujanja ujanja pia hujifunza hali ya udokozi na wizi kulinganisha na makundi mengine.
vii. Wazazi katika kundi hili hutafuta makosa na kuyashughulikia kuliko mema.
viii. Wazazi katika kundi hili huwa hawana maneno ya kutia moyo hata kama siku mtoto atafanya vizuri mzazi atamezea tu moyoni lakini kamwe hatamsifia wala kumpongeza mtoto.
ix. Watoto katika kundi hili huwa na nidhamu ya uwoga na sio nidhamu ya kweli.
x. Wazai mliopo katika kundi hili mnahitaji sana neema ya Mungu maana anabomoma maisha ya watoto na kuna athari nyingi zitajitokeza wakati wa utu uzima wa hawa watoto.

Kundi - 4
Wazazi wenye USHIRIKA NA WATOTO
i. Wanaonyesha upendo kwa watoto.
ii. Hufundisha mtoto mambo ya kushika na mambo ya kuyaepuka.
iii. Huonyesha kuunga mkono mambo mazuri yanayofanywa na mtoto.
iv. Humuadhibu mtoto ipasavyo pale anapokuwa amekosea na humweleza mtoto kwanini anaadhibiwa.
v. Humueleimisha mtoto kuwa adhabu anayoipata ni kwafaida yake mwenyewe ili kuondoa uharibifu ndani yake.
vi. Wazazi katika kundi hili, hujenga mawasiliano mazuri baina yao na mtoto.
vii. Hutumia muda mwingi kuwa na watoto ili kugundua baadhi ya tabia ambazo huwezi kuzigundua kwa mtoto kama utakuwa mbali naye.
SIJUI MSOMAJI MPAKA HAPA UMEPALIKIWA NA POINTI YA NGAPI NA UTAKUWA UMEJIJUA WEWE UPO KUNDI GANI

Comments