MAMIA WAZIDI KUMIMINIKA KANISA LA UFUFUO ARUSHA, MISS REDDS MMOJA WAO

Kanisa la Ufufuo na Uzima mkoani Arusha, limeendelea kujikusanyia mamia ya waumini kila jumapili, kutokana na moto wa injili unaowashwa kanisani hapo, kupitia mchungaji kiongozi Frank Andrew pamoja na mwimbaji marrufu nchini Jackson Benty ambaye huongoza sifa na kundi la Platform la kanisa hilo jijini humo.

Tangu kuanza kwa kanisa hilo mapema mwaka jana mara baada ya mkutano mkubwa uliovunja rekodi ya mahudhurio na matendo makuu yaliyodhihirika ndipo kanisa hilo likaamua kuwepo na tawi lao mkoani humo, huku mmoja kati ya wahudhuriaji katika mkutano huo alitoa kiwanja chake kitumike na kanisa hilo ambalo mpaka sasa limeendelea kusimama na waumini kuendelea kuongezeka kila iitwapo leo.

Kati ya matukio yaliyojitokeza katika ibada ya jana ni pamoja mama Asnath Terevaeli alikabidhi mikufu yake (shanga za shingoni) madhabahuni kutokana na mikufu hiyo aliyopewa na mwanae ilikuwa ikimtesa kila alipokuwa akiivaa. Aidha katika tukio lingine aliyekuwa mlimbwende kupitia shindano la miss Tanzania kipengele cha kinywaji cha Reds aliamua kumpa Yesu maisha yake. Tazama baadhi ya picha za ibada ya jana kama zilivyotolewa na Ufufuo crew ya kanisa hilo.

Jackson Benty akiongoza sifa kanisani hapo.
Platform ya Ufufuo Arusha wakimpa Mungu utukufu.
Aliyekuwa miss Reds Arusha akifanyiwa maombi kanisani hapo na mchungaji Frank Andrew.
Mama Asnath akirudisha kanisani shanga alizopewa na mwanae kama zawadi kwakuwa zimemtesa kwa muda mrefu.
Maombi yakaanza.
Uweponi mwa Bwana.
Mamia ya waumini wakiwa katika maombi.

Comments