
Hii imemtokea Mtume Peter Nyaga baada ya kufanya kazi ya Mungu kwa uaminifu mkoani Morogoro, mkutano ulioandaliwa na Mwinjilisti Jailos Maloda, Mungu aliweza kuwatumia maasai ambao walijitokeza na kusema wamebarikiwa sana na mahubiri yake na hii iliwafanya watoe mbuzi za nguvu kama zwadi kwake.
Kwa kupitia ushuhuda huu unajifunza nini mtu wa Mungu? Mtume Peter Nyaga wakati anatokea Dar es Salaam hakutegemea kupokea mbuzi lakini baada ya kumaliza kazi ya Mungu aliweza kupokea ujira wake. Nachotaka kusema kwako ni kwamba, FANYA KAZI YA MUNGU KWA UAMINIFU NA JITAHIDI KUWA MWAMINIFU KWA KUFUATA AMRI KUMI ZA MUNGU
Comments