MUNGU NI BABA YETU MZAZI

Yakobo 1:18
"Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyote."

Watu wengi sana wanamuita Mungu ni Baba yao, lakini hawajui kama ni "Baba Mzazi".
Mungu ametupatia somo hili kwa makusudi kabisa ili watu wajue nafasi ya Mungu kwa watu wake aliowanunua kwa damu yake ya thamani.


Biblia inatuthibitishia hili, kwa kusema "ALITUZAA SISI KWA NENO LA KWELI", sasa tunaweza kuelewa vizuri kwa nini Biblia inasema; "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake" Yoh 1:12

Kumbe, Wote waliompokea Yesu yaani waliookoka ndio watoto hasa wa Mungu ambao biblia inasema aliwazaa kwa neno la kweli.
Kama Hujaokoka yaani hujampa Yesu Maisha yako, Mungu si Baba yako Mzazi....


Lakini hujachelewa bado unayo nafasi!!
Haleleyaaaaa........

Neno Mzazi, ndilo linaonesha nafasi ya Mungu kwa Mtu aliyeokoka.
Hebu tuangalie mfano wa kawaida kabisa katika maisha yetu, ili tuone uzito wa neno MZAZI.


Pengine kuna mtu au watu kwenye maisha yako Unamuita Baba na Yeye anakuitikia vizuri kabisa, Lakini kama sio Baba yako MZAZI lazima kuna vitu hawezi kukushirikisha, au hata ukimuomba asikupe.


Sio, kwa sababu hakupendi bali kwa sababu Sio Baba yako MZAZI.

Unaweza kulitumia somo hili kwenye Maombi, Umeshajua kwamba Mungu ni Baba yako Mzazi, na wala sio baba wa kambo au Mababa wengine wa Mtaani. Kwa hiyo uwe na uhakika kwamba, Lazima atakupatia tu kwa vile wewe ni Mtoto wake wa Kukuzaa!!
Hebu, tuendelee kuyachunguza Maandiko kama wale watu wa Beroya (Mdo 17:11) ili tuone Msisitizo uliopo kwenye Jambo Hili.
Yesu alimuita Mungu wa Mbinguni "ABA", neno hilo likiwa na Maana Baba! Na neno hilo lilitumika kwa Baba wa familia tu, na si kwa Baba mwingine yeyote (Aba neno la Kiaramu)
Hebu tusome "Akasema, Aba, Baba, yote yawezekana kwa;...." Marko 14:36
Umeliona hilo!? Yesu alilitumia kwenye Maombi yake, ili kuonyesha nafasi aliyonayo Baba yake kwake, ili aweze Kumjibu Kama Baba kwa Mtoto. Hata wewe unaweza ukaomba hivyo.....

Bwana Yesu asifiwe sana.....

Angalia kwetu sisi pia tulioliamini Jina La Yesu!
"Kwa kuwa hamkupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu; bali mlipolea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba." Rumi 8:15

Siumeona hayo maandiko, hebu yasome tena na uyatafakari vizuri!, ruhusu Roho Mtakatifu akufunulie kilichijificha ndani yake!!
Pia onganisha na WAGALATIA 4:6

Mungu akubariki sana wewe uliyepata neema ya Kulisoma somo hili, ambalo Mungu ametupa!!

Mungu akikupa neema Rudia tena na tena kulisoma hapahapa . pia Ulitafakari vizuri!!

Kama hujaokoka, Amua Leo kumbuka kwamba saa ya Wokovu ni sasa!!
Amen, amen!!!.

 Mungu akubariki sana kwa JINA LA YESU!!.
By  Nickson Mabena

Comments