Mwimbaji Darlene Zchech apanda jukwaani kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza matibabu


Hatimaye Mungu amesikia maombi ya watu wake baada ya mwimbaji wa zamani wa kanisa la Hillsong mwanamama Darlene Zschech kumaliza matibabu ya kansa ya titi aliyoanza mwezi disemba mwaka jana na hapo jana kufanikiwa kupanda madhabahuni kwa mara kwanza toka aanza matibabu ya ugonjwa huo unaomaliza wengi.
Mwanamama huyo alitangaza tendo hilo kubwa alilotendewa na Mungu wiki hii kwakushukuru maombi ya watu waliokuwa pamoja naye bega kwa bega na kwamba hapo jana ilikuwa siku yake ya kwanza kurejea madhabahuni kumtukuza Mungu katika kanisa wanaloongoza na mumewe Mark liitwalo Hope Unlimited, toka aanze matibabu. 
Darlene akiongoza sifa  kanisani kwake.
Ambapo baada ya kumaliza na matibabu hayo kwasasa mwanamama huyo anatarajia kuanza kupiga mionzi ili kumaliza kabisa chembechembe za ugonjwa huo katika mwili wake.

Darlene anatambulika kama kiongozi wa muziki wa kisasa zaidi makanisani linapokuja suala la kusifu na kuabudu toka awe chachu ya mabadiliko ya muziki makanisani kupitia kanisa lake la zamani la Hillsong ambalo bado linasonga mbele na kushika nafasi za juu kwenye makanisa yanayopendwa kwa kuwekeza vyema kwenye muziki wa kisasa wa kumuinua Mungu.


credits:gospel kitaa

Comments