NDUGU ZANGU WALINITENGA KWA SABABU YA MAGONJWA LAKINI BAADA YA YESU KUNIPONYA WAMENITENGA TENA BAADA YA KUBADILI DINI.


ushuhuda unaogusa sana ukiendelea.
BWANA YESU anaposema ''Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.-Mathayo 11:28'' anauhakika na kutupumzisha, hakuna la kumshinda yeye na matendo yake ni makuu sana,
Nimetembelea kihuduma katika kanisa la Pentecostal Assemblies of GOD Chalinze na kuyashuhudia matendo makuu ya MUNGU.
Mama huyu aliyebadili dini na kuwa mkristo baada ya kutaabika kwa mika 20 bila kupona , na kilichonifurahisha zaidi ni pale mama huyu alipompa zawadi Askofu Thomas Dige ambaye ndio aliyemuombea mwaka 1 na nusu uliopita.

Mama huyu alikuwa na tatizo la kusikia, tumbo lake lilijaa vidonda vya tumbo, alikuwa anajisaidia mara nyingi kupita kawaida  haja kubwa na tena alikuwa kikojozi kwa miaka 20 na hali hiyo ilipelekea kutengwa na ndugu zake wote.


Ndugu zake walifikia hatua ya kusema kwamba wao hawana ndugu wa aina hiyo  na kumtenda vibaya , alijaribu kutafuta tiba lakini hakupona kwa miaka 20, alienda hospitali kubwa ikiwemo hospitali ya taifa lakini hakupona wala kupata nafuu.
Mwaka jana wakati Askofu Dige anafanya mkutano wa injili huko chalinze mama huyu aliona ngoja amkabidhi BWANA YESU maisha yake. Alipofika kwenye mkutano wa injili aliombewa na mapepo yakamtoka. Baada ya maombezi Askofu Dige alimwambia kwamba aende akale maharage ambayo ameyamisi kwa miaka mingi na hiyo ndio itakuwa uhakikisho wa uponyaji wake. mama huyu alitii na kwenda kula lakini cha ajabu hakudhurika kama ilivyokuwa awali. na hakika alipona kabisa.
YESU anaokoa, ukiamini unaokoka. Licha ya kupona vidonda sugu  vya tumbo BWANA alimponya na magonjwa yote.
Kitendo cha kupona na kuanza kwenda kanisani ndugu zake walikuja juu na kumwambia haiwezekani kuiacha dini na kumpokea BWANA YESU. Mama huyiu aliwashangaa ndugu zake ambao walimtenga kwa miaka mingi leo wanamwona wa muhimu baada ya kuokoka , hii ni ajabu hata hivyo mama huyu aliendelea na YESU hadi leo. Ndugu wamemtenga tena lakini kipindi hiki hawajamtenga kwa sababu ya ukikojozi bali wamemtenga kwa sababu ya kuijua kweli ambayo imemweka huru.
Tuliambata na Askofu Dige katika ziara ya jimbo ya idara ya vijana, na Askofu alisema machache baada ya mama huyo kutoa ushuhuda wake, akimwambia asonge mbele na BWANA YESU mwenye uzima.
Hakika KWA YESU KRISTO YOTE YANAWEZEKANA na BWANA YESU alidhihilishwa ili azivunje kazi za shetani( 1 Yohana 3:8b).
Nampenda BWANA YESU maana anaponya na kuwaweha huru wote waliomwendea.
Mama akishuhudia na kumshukuru sana MUNGU kwa kuwatumia watumishi wake kuleta uzima kwake.
Askofu Dige akisisitiza jambo baada ya mama kumaliza kushuhudia.

Comments