NILICHONACHO NDICHO NIKUPACHO.


" Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka.
Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi.
Akawaangalia, akitaraji kupata kitu kwao.

Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.
Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu.
Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu Mungu. " Matendo 3:6-8

Haleluya...
Petro akasema " Mimi sina fedha,wala dhahabu,lakini nilicho nacho ndicho nikupacho Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,simama na uende "
Alichonacho Petro ni Yesu Kristo wa Nazareti tu,na ndicho alichompa.
Haleluya...
Kanuni ya utoaji inasema;
• Huwezi kutoa kile usichonacho.Siku zote hutoa kile ulichonacho tu.
Na Mtumishi Gasper Madumla
Mfano;
Ukimuendea mtu na kumwambia akupe tshs million moja,na ikiwa kama hana,basi ujue hawezi kukupa kamwe,zaidi sana atakuzungusha tu,sababu hana. Ulichonacho ndicho hutoacho.
Kama Petro angelikuwa na pesa na dhahabu yamkini angelitoa,lakini hakuwa navyo vyote hivyo,bali alikuwa na UPAKO,yaani Yesu Kristo tu.
Na ndio maana akatoa kile alichonacho.Leo hii nami sina pesa wala dhahabu,bali nilichonacho ndicho hiki nikupacho,kwa Jina lake Yesu Kristo wa Nazareti upokee neno la Bwana na likuweke huru.
Sema AMEN...

Maandiko matakatifu tuliyoyasoma hapo juu,yanatufundisha kwamba hakuna lisilowezekana kwa Mungu,yaani kile alichokishindwa mwanadamu kwa Mungu kinawezekana.
Biblia inasema;
Yule kiwete hakuwahi kwenda kabisa,maana ndivyo alivyozaliwa toka tumboni mwa mamaye (Matendo 3:2).
Lakini;
Kwa mara ya kwanza akatembea pale alipokutana na Yesu ndani ya Petro.

Yapo mambo yanayoonekana kwa macho yetu ya damu na nyama kwamba hayawezekani kabisa kama vile jinsi alivyokuwa akijiona yule kiwete pamoja na wale waliomchukua na kumuweka katika mlango wa mzuri.
Watu hawa waliomchukua kiwete na kumuweka mlangoni mwa hekalu waliamini hatapona kwa kutembea kwa miguu yake mwenyewe ndio maana waliamua wamuweke ashinde pale mlangoni kwa kuomba sadaka siku zote.
Lakini kumbe hali haikuwa hivyo,maana Mungu hutuwazia mawazo mema siku zote,anasema;
" Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. " Yeremia 29:11
Andiko hili,nalipenda jinsi linavyosema katika Biblia ya kiingereza ya Amplified bible,inasema;
" For I know the thoughts and plans that I have for you, says the Lord, thoughts and plans for welfare and peace and not for evil, to give you hope in your final outcome. " Jeremiah 29:11
Neno " mawazo" anayotuwazia Bwana Mungu limepanuliwa kwa kuelezwa kuwa ni " plans" yaani "mipango"
Hivyo mipango anayotupangia Bwana Mungu ni " mipango" (plans) ya AMANI isiyo ya kishetani,isiyo mipango mibaya. Mungu siku zote hutuwazia mema watu wote,wema na wabaya pia. Hata kiwete huyu,aliwaziwa mema.

Sasa angalia;
Bwana Mungu akatuma neno lake kupitia Petro ili limponye kiwete.
Yamkini unafanana na huyu kiwete kwa habari ya maisha yako.
Lakini mimi nataka nikutangazie UZIMA WA KWELI kupitia jina la Yesu Kristo wa Nazareti.Nina uhakika na hiki nikuambiacho,la kama sina nisingekuambia leo hii.

Haleluya...
Unajua huyu kiwete alikuwa akiwekwa pale mlangoni mwa hekalu siku zote akipata sadaka za watu. Maisha ya sadaka hayakumsaidia;
Maana yalimfanya awe omba omba siku zote.Mungu hakukusudia awe omba omba,bali aponywe na hiyo hali aliyokuwa nayo.

Petro na Yohana wana uhakika na Mungu wao wanaomtumikia, hiyo ndio IMANI halisi. Laiti kama Petro asingekuwa na uhakika wa uponyaji wa kiwete basi labda angelisema " kijana ngoja nikatafute pesa kidogo ya kukupa alafu Mungu wako atakuponya " Lakini tazama Petro anasema kwa ujasiri uponyaji mkuu kwa jina la Yesu Kristo.
Kwa lugha nyingine ni kwamba,Petro hakupenda yale maisha ya kuomba omba,ndani yake alisikia Yesu akamponya yule alikuwa kiwete.
Bwana Yesu asifiwe....
Jina la Yesu linaponya,
Lina ushindi,lina uhisha,
Na linatupa uhai mpya kabisa...
Yesu yule yule aliye mponya kiwete hata kutembea,ndio Yesu huyu ninaye muhubiri hivi sasa,naye atakuponya wewe uaminiye.

Hivi unajua,
Hata madaktari hawawezi kuponya. Sababu mtu hutoa alichonacho,kile walichonacho madaktari ni TIBA hivyo wao hutoa TIBA maana ndicho walicho nacho,
Bali Mungu huponya maana hutoa UPONYAJI.
Ipo tofauti kubwa kati ya TIBA na UPONYAJI
• Tiba hutolewa na daktari,kwa vipimo vyake kwa kadri ya elimu yake
• Uponyaji hutolewa na Mungu kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti. Uponyaji wa Mungu huwa ni halisi.

Leo hii Yesu Kristo yu hai halisi kabisa,ukiamini hiki nikuambiacho UPONYAJI ni sehemu yako.
Petro alitumia kanuni ya Ki-Mungu maana aliongozwa na neno hili;
" kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. "Warumi 10:13
Kuokoka kwa yule kiwete ilikuwa ni kuliitia jina la Bwana tu,Petro alipogundua hilo akaliitia jina la Bwana akasema Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,simama uende,naye akaenda sawa sawa na neno la Mungu.
Haleluya...
Aahaa!
Nampenda Yesu jamani,
Ameniokoa hata mimi,kwa jina lake tu..

Ndani yangu injili ya kweli,halisi inachemka,sababu UPONYAJI,MAISHA YA KWELI,UZIMA UPO NDANI YAKE BWANA,ukilijua hili utakuwa umepata faida kubwa sana.
Ngoja nijaribu tena hivi;
Uponyaji wa Bwana Yesu hulikwisha achiliwa pale msalabani kwako pamoja na kwangu pia( 1 Petro 2:24) Tunachokifanya sasa ni kujiungamanisha na uponyaji huo.
Uponyaji wa Bwana Yesu ni kwa kila magonjwa,udhaifu hata ulemavu wa aina yoyote ile.

Haleluya,...
Haleluya....

Siku ya leo,maji yameshatibuliwa;
Uponyaji upo hapa hapa,
Usisite kunipigia simu ili tukaliitie jina la Bwana Yesu,naye akuponye..

Je una amini hayo?
Ikiwa jibu ni ndio,basi piga namba yangu hii;
0655-111149

UBARIKIWE.

Comments