NINI KINACHOONGOZA MAISHA YAKO.

Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.

Maisha ya kila mtu yanaongozwa na kitu flani.
Je, ni nguvu gani inayoongoza maisha yako?
sasa hivi unaweza kuongozwa na tatizo ,msukumo flani, au tarehe ya
mwisho kwa kitu flani .Unaweza kuongozwa nakumbukumbu ya jambo flani linalo umiza ,hofu mbaya ,imani ya ndani. Hapa kuna mambo matano ambayo ni ya kawaida kwa wengi .



Watu wengi huongozwa na hatia: Watu hawa hutumia muda wa maisha yao yote wakiepuka lawama nakuficha aibu. Watu wanaoongozwa na hatia wanaongozwa sana na kumbukumbu wanaruhusu mambo yaliopita kutawala mambo yao ya usoni wanajiadhibu bila kujua kwa kuharibu mafanikio yao.Kaini alipotenda dhambi,hatia yake ilimtenga na Mungu. Kusudi la Mungu alifungwi na muda wako uliopita. Mungu ni mtaalamu wa kuwapa watu mwanzo mpya.

Watu wengi wanaongozwa na chuki na hasira:Watu hawa wanashikilia maumivu (machungu bila kuyaacha .Badala ya kutoka katika maumivu kwa kusamehe ,wanaendelea kuyakumbuka katika mawazo yao.Watu wengine wanaongozwa na chuki hutunza ndani uchungu wao na wengine huwalipukia watu wengine.Hali zote hizi si nzuri na wala hazisaidii maishani. Biblia inasema, Kuwa na hofu kiasi cha kufa kwa sababu ya uchungu ni upumbavu ,ni kitu cha kipumbavu kukifanya.

Watu wengi wanaongozwa na woga: Watu wanaoongozwa na woga mara nyingi hupitwa na nafasi kubwa kwa sababu wanaogopa kuchukua hatua.Woga ni kifungo ambacho mtu hujifunga mwenyewe na chaweza kukuzuia kuwa mtu yule ambaye Mungu anapenda uwe.Unatakiwa utoke humo kwa njia ya silaha ya imani na upendo. Biblia inasema, Upendo halisi huindoa hofu , kwa kuwa hofu hulemaza maisha ya hofu, hofu ya hukumu ni maisha ambayo hayajakamilika katika upendo.

Watu wengi wanaongozwa na mali:Tamaa ya kupata vitu linakuwa ndilo Lengo la maisha yao yote.Utajiri unaweza kupotezwa mara moja kwa sababu zisizozuilika,usalama halisi unaweza kupatikana katika kile ambacho huwezi kunyanganywa yaani uhusiano wako na Mungu.

Watu wengi wanaongozwa na kutaka sifa:Watu hawa hawa wanaruhusu matarajio ya wazazi ,waume,wake,watoto, waalimu,au marafiki zao kutawala maisha yao. Kuna nguvu zingine zinazoweza kutawala maisha yako lakini zote mwisho wake ni mfu,bila Malengo maisha ni mwendo usio na maana ,shughuli bila mwelekeo,na matukio bila sababu,bila malengo, maisha ni kitu duni,kisicho na umuhimu wowote.Biblia inasema, hakuna mtu anaweza kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.

Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292

Comments