NJIA 7 KUUJUA UPENDO WA KWELI.

Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.

(i) Haukati tamaa,umejaa amani,furaha na kuvumiliana siku zote kwa hali zote(1Wakorintho13:4-8-Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;  haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;  haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. )

(ii)Haujisumbui kwa kile usicho nacho.


(iii)Husaidia wengine,hutoa hisani bila masharti.


(iv)Huumia kwa maumivu ya wengine,haukomoani wala haufurahii mateso kwa wengine.


(v)Hautukani,hauhifadhi mabaya,haukumbuki majeraha ya zamani,hauwashuku wengine!Haujawi na tamaa wala majivuno.
(vi)Hauna ubinafsi wala choyo.


(vii)Hudumu siku zote hata kama unapita katika nyakati ngumu na nzito,daima upendo hustahimili.


Amani ya BWANA iwe nawe.

Nakutakia upendo wa kweli ndani yako,upendo udumuo,usiokata tamaa wala kuchujuka kwa jina la Yesu.

 
Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.
Kwa Mobile +255(0)7 (57/84) 464 141/ 12 909 021.
Au Email sos.sesi@yahoo.com / newelshaddai@gmail.com

Tunakushauri, utembelee kanisa la kiroho lililo jirani yako, kwaajili ya mafundisho zaidi na Ushirika. (Kumbukumbu la Torati 28:6).

Comments