Papa Francis, Waziri Mkuu Israel walumbana kuhusu YESU KRISTO.


Papa Francis
Malumbano makali ya maneno na hoja yamezuka baina ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuhusu lugha gani aliyotumia YESU KRISTO  miaka 2,000 iliyopita. 

Viongozi hao Jumatatu mchana wakati wa ziara ya siku tatu ya Papa aliyoifanya katika eneo la Mashariki ya Kati ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu atwae wadhifa huo.

 “YESU aliishi hapa katika ardhi ya nchi hii. Alizungumzia Kiebrania,” alianza Netanyahu wakati akimweleza Papa Francis kwenye mkutano wa hadhara mjini Yerusalemu.

Netanyahu, pia akaeleza kuwa upo uhusiano wa karibu baina ya mahali alikozaliwa YESU na Ukristo.

Naye Papa Francis akasikiliza kwa muda, kisha akajibu: “YESU alizungumza lugha ya Kiaramaiki.”

“Ndiyo, nimesema alizungumza Kiaramaiki, lakini pia alijua Kiebrania,” akaingilia kati Netanyahu.

Hata hivyo, mjadala huo umepokewa kwa hisia tofauti na watu wengi ambao wamekuwa wakifuatilia ziara ya siku tatu ya Papa Francis katika nchi takatifu.

Mtaalamu wa masuala ya lugha, raia wa Israel, Profesa Ghil’ad Zuckermann ameliambia Shirika la Habari la Reuters kwamba wawili hao, Netanyahu, ambaye ni mtoto wa mtaalamu wa historia ya Kiyahudi na Papa Francis, kiongozi wa kiroho anayeongoza waumini bilioni 1.2 Wakatoliki, kila mmoja ana hoja. “YESU alikuwa mzungumzaji wa Kiaramaiki,” anasema Profesa Zuckerman kuhusu lugha hiyo ambayo imetoweka yenye uhusiano na Kiebrania. “Pia, anaweza kuwa alizungumza na kufahamu Kiebrania, lugha ambayo ilitumika kwenye maandiko.”

Prof Zuckermann alisema kuwa wakati wa YESU, Kiebrania kilizungumzwa na watu wa madaraja ya chini - “ambao ndiyo aliowahubiria”. Mojawapo ya vitu vingi katika eneo la Mashariki ya Kati hadi sasa ni kuhusu utata wa YESU, utata huo umechukua pia sura na mtazamo wa kisiasa.

YESU alizaliwa kwenye mji wa Bethlehemu ambao ulikuwa chini ya himaya ya Warumi, kwenye Mkoa wa Yudea, katika ardhi inayoshikiliwa kwa sasa na Israel kwenye Ukanda wa Magharibi.

Alikulia mjini Nazareth , akaendesha utume kwenye mji mwingine wa Galilea, ambao pia uko kaskazini mwa Israel, alikufa na kufufuka mjini Yerusalemu, mji ambao unatukuzwa na Wayahudi, WAKRISTO na Waislamu, ambao unagombewa na tawala za Israel na Palestina hadi sasa.


Kwa upande wao, Wapalestina wamekuwa wakidai kuwa YESU ni Mpalestina. Hata hivyo, utawala wa Israel umekuwa ukipingana na mtazamo huo.


Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.


KUTOKA KWANGU.
Ukitaka kujua kwa undani kuhusu BWANA YESU na lugha alizotumia akiwa hapa duniani soma BIBLIA.
BWANA YESU akubariki na anakupenda.
Na WOKOVU wa kweli hutoka kwake tu.

Comments