REV BEN AONYESHWA MAONO YA VITA KATIKA NCHI YA TANZANA MAOMBI YAHITAJIKA KUNISURU

Mchungaji Kiongozi wa huduma ya Assaph Ministries International Rev Ben, hivi karibuni alionyeshwa katika maono nchi ya Tanzania ikiwa katika vita kubwa. Mtumishi amesema hii ni Mara ya tatu sasa anaonyeshwa na hii imekuwa ni kubwa hata kumfanya baada ya kutoka kwenye maono hayo moyo kumwenda mbio. Alieleza aliona jinsi watu watakavyopata shida katika kukbia hasa watoto akina mama na wazee.


Ikumbukwe miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mivutano mbali mbali ya kisiasa na mihemuko ya wanajamii katika sehemu mbalimbali na kusababisha hata baadhi ya watu kupoteza maisha bila hatia lakini pia kumeongezeka maasi yanayotokana na kuporomoka kwa maadili na mabaliko ya kijamii yatokanayo na utandawazi. 

Lakini kumekuwa na mihemuko ya kidini sehemu ambayo imesababisha vurugu za hapa na pale na hata watu kumwagiwa tindi Kali na utumiwaji wa siraha za moto kama risasi na mabomu. Katika maelezo Yake amesema kuna msukumo wa chini kwa chini kutoka nchi nyingine kwa kutaka kuharibu tu amani iliyopo Tanzania. Wanajiuliza kwanini Tanzania iwe na amani tuuu wanaweza hata kutumia pesa kuwatumia baadhi ya watanzania kutuvuruga, aliuliza kama Tanzania kutatokea vita tutakimbilia wapi? Maana majirani wote wanaotuzunguka si swali. Alimaliza kwa kusema anatamani watanzania wapate ujumbe huu ili kwa pamoja tuungane kuombea amani nchi yetu ya Tanzania.

 Mungu anasema katika kitabu cha 2nyakati 7:14  Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuiponya nchi yao.  hivyo hata mtu mmoja akimaanisha basi Mungu yuko kusikia na kughaili hivyo watanzania tunahamasisha kuiombea inchi Yetu ili Mungu atunusuru na vita.

Ikumbukwe huko nyuma kulikuwa na huduma ya Tanzania itubu ambayo ilihamasisha watanzania kutubu ili tusipatwe na majanga ni wakati wa kumrudia Muumba wetu ili aiponye inchi yetu.

Comments