SAFARI YETU YA ZANZIBAR.

Bandarini Zanzibar.
BWANA YESU asifiwe.
Siku chae zilizopita nilisafiri kwenda Zanzibar kihuduma, mimi pamoja na Askofu Joseph Masanja na Pamoja na Mchungaji Lucas Mpenzile. Lengo la kwenda huko ilikuwa ni kwenda kuwatia moyo vijana wa kanisa la Pentecostal Assemblies of GOD(P A G)T. Askofu Msanja ni Mkurugenzi wa taifa wa idara ya vijana ya kanisa, Mchungaji Lucas Mpenzile ni Mkurugenzi wa jimbo ambalo ni mikoa 9 ya kiserikali na mimi ni katibu wa jimbo.
Nimejifunza mengi sana Zanzibar.
-Kwanza wateule wa BWANA YESU ni wengi sana huko kwa sasa.
 -Injili inasonga mbele.
 -Watu wanaompokea BWANA YESU kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yao.
-MUNGU anajibu maombi ya watumishi wake.
Hizi ni baadhi ya picha katika safari hiyo.
Endelea kuombea kanisa na endelea kujitoa kwa ajili ya kupeleka injili duniani.




Bandarini kabla ya kuondoka.

Nikiwa na Askofu Joseph Masanja ndani ya Boti.

Mtumishi wa MUNGU, Mchungaji Lucas Mpenzile ndani ya boti kuelekea Zanzibar.

Wenyeji wetu ni wakarimu sana  walituandalia usafiri mzuri wa kutupeleka sehemu ya kufikia.

Kutoka kulia ni mimi Peter Mabula, Askofu Masanja, Pastor Mpenzile na mwenyeji wetu mkurugezi wa vijana Zanzibar Nehemia Msaghaa.

Hapa ni kanisani Chukwani, P A G vijana choir wakimtukuza MUNGU.

SALAMU KUTOKA KWA WATU WA MUNGU WA ZANZIBAR.


HII NDIO ILIKUWA TIMU YETU, ASKOFU MASANJA, MCHUNGAJI MPENZILE NA MIMI.

Ni furaha kuwa ndani ya YESU KRISTO.

Nikiwa na Mwinjilisti Isaya Chubulilu ambaye anamtumika MUNGU huko Zanzibar, mtumishi huyu huhubiri kanisani na hata mitaani na kwa habari ya midahalo hapa ndio kwenyewe.

Nikiwa na mkurugenzi wa vijana Zanzibar, Nehemia Msaghaa.

Nikiwa na mtumishi wa MUNGU Zakaria Benjizoba.

nikiwa na wateule wa BWANA YESU huko Zanzibar.

Namshuru BWANA YESU kwa neema hii.

Niliwahi kukaa Zanzibar miaka 5 na Mwimbaji huyu alikua mtoto mdogo lakini kwa sasa ni mwimbaji wa kiwango kikubwa sana.

Nikiwa na watumishi wa MUNGU, Maria na Baraka mhuda ambaye pia ndio mwenyekiti wa kwaya.

Zakaria akinikaribisha.



Tumerudi kutoka Zanzibar na hapa tumefika nyumbani Dar.

Bandarini Dar panaonyesha kabisa umeingia sehemu ambapo BWANA YESU anaokoa, ukiamini unaokoka.

Comments