Somo : WALIDHANI UTAKUFA GHAFLA

Na Senior Pastor.JOHN KILIMA, UFUFUO NA UZIMA TANGA.
Matendo 28:1 "Tulipokwisha kuokoka,ndipo tulipojua ya kuwa kisiwa kile chaitwa melita"
Naliposoma andiko hili nikafahamu ya kuwa mungu huruhusu jambo fulani baya likupate ili apate kukuvusha kutoka hatua moja kwenda nyingine.
Kila tunapoendelea kujifunza neno la mungu ndivyo tunaendelea kusonga mbele.
         
Mashindano ya dini yanaweza kutokea kama tukitazama katika kitabu cha matendo ya mitume :25:19"bali walikuwa na maswali mengine mengine juu yake katika dini yao wenyewe,na katika habari ya mtu mmoja anaitwa Yesu, aliyekwisha kufa,ambaye paulo alikaza kusema  yu hai". Kwa hiyo unaweza kupata  tatizo fulani,kwa ukiri wako wa kuwa Yesu Kristo ni Bwana na mwokozi wa maisha yako na alikufa na akafufuka yu hai leo hata milele.
Hivyo tunapokumbana na mikasa hiyo inabidi kusonga mbele kwa imani ile ile.
Pia tukisoma kitabu cha nabii Isaya:10:26 imeandikwa"Na Bwana wa majeshi ataamsha mijeledi juu yake.Kama vile alivyopiga midiani karibu na jabali la Orebu na fimbo yake itakuwa juu ya bahari,naye ataiinua kwa namna ya kimisri".
Kwa hiyo unapoendelea kusonga mbele  kwa nguvu na kupambana kwa imani ile katika ulimwengu wa roho , mungu mwenywe ambaye ni bwana wa majeshi atafanya vita  nao kwa namna ya ajabu! Tena bwana asema katika Isaya:10:27"Tena katika siku hiyo mzingo wako utaondoka begani mwako,na nira yake shingoni mwako,nayo nira itaharibiwa kwa sababu ya kutiwa mafuta".
Neno nira ni kama vifungo vyaweza kuwa vya mbao au chuma ili kwamba ufungwapo usitoke na ubaki katika milki yao lakini Bwana wa majeshi  asema haijarishi ni nira ya namna gani itaharibiwa kwa kutiwa mafuta.
Kwa maana imeandikwa katika Waefeso:6:12"kwa maana kushindana kwetu sisi si juu yadamu na nyama;bali juu falme na mamlaka,juu ya wakuu wa giza hili,juu ya majeshi ya pepeo wabaya katika ulimwengu wa roho". Kwa hiyo haya ni majeshi yanayo tufatilia na inabidi tufanye vita nayo,tupambane nayo,tushindane nayo kwa jina la yesu na kwa kuwa imeandikwa nao wakamshinda kwa damu ya mwana kondoo.
Vilevile  tunaposhinda katika vita hivi dhidi ya  ibilisi na majeshi yake Bwana Yesu Kristo yuko pamoaja nasi kwa kuwa Mungu ni Bwana vita kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Joshua:5:12"Ikawa  hapo Joshuwa alipokuwa karibu na mji wa Yeriko,akavua macho yake na kuangalia,na tazama mtu mume kasimama  kumkabili mbele yake ,naye alikuwa na upanga wazi mikononi mwake,Joshua akamwendea  na kumwabia Je!wewe u upande wetu au upande waadui zetu?Akasema la! Lakini nimekuja sasa,nili amiri jeshi la Bwana.Yoshua akapomoka kiusouso hata nchi,naye akasujudu,akamwambia Bwana wangu ananiambia nini mtumishi wake?".
Katika Matendo:28:3,5"Paulo alipokuwa amekusanya mzingo wa kuni na kuweka motoni,nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto akamzongazonga mkononi. Lakini yeye akamtukusia motoni asipate madhara wao wakadhani atavimba au kuanguka chini kwa kufa ghafla na wakiisha kumwangalia halimpati dhara lolote wakageuka na kusema yeye ni mungu".
Kwa hiyo kwa ushuhuda wa maisha yako katika Kristo Yesu wengine wanapata kuacha maisha ya dhambi na kumgeukia Mungu.Na dhara halikumpata Paulo, hivyo hatupaswi kuishi katika vifungo vy a shetani,umaskini,mogonjwa ,kufa ghafla,kukosa kazi,kurogwa na hivyo ni muhimu sana kuwapiga walinzi wangome kama vile kutokuamini,hofu,wasiwasi ni walinzi wa ngome hao kama ilivyoandikwa katika Matendo ya Mitume :4:1"hata wlipokuwa wakisema na watu wale,makuhani na akida wa hekalu na masadukayo wakawatokea".hii ina maanisha ni walinzi wa ngome hao hawataki ukombozi hao.
Hivyo nini hasa cha kufanya?.Ila katika hili tunayo amri  kama ilivyoandikwa katika matendo ya mitume:10:1,16,:6:7,:16:15 kwa hiyo tutakalonena ndilo litakwa.
Ndugu tunapaswa kumshinda shetani katika roho  kwa jina la Yesu.
Amen.

Comments