TANGAZA MSIMAMO WA WOKOVU WAKO..


"Mdo 5:27-29 Walipowaleta wakawaweka ktk baraza, kuhani mkuu akawauliza akisema, je hatukuwaamuru ninyi msifundishe kwa jina hili?, nanyi tazameni mmeijaza Yerusalem mafundisho yenu na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu, Petro na mitume wakajibu wakisema imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu". 

Biblia inaeleza habari za mitume jinsi walivyosimama kwa imani katika kutangaza msimamo wa wokovu na kuliinua jina la KRISTO YESU. 

 Petro na mitume wengine wakimwambia kuhani kuwa imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu, petro na mitume wanaonyesha msimamo wa wokovu wao. 

Mara nyingi watu wamekuwa wakishindwa kutangaza msimamo wa wokovu wao kwa sababu ya

 (1)UOGA,

 (2)WASIWASI, 

(3)MASHAKA, 

(4)KUTOKUWA NA IMANI NA KILE WANACHOKIAMINI, 

(5)KUTOKUWA NA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU, 

(6)KUTOLIJUA NENO,

 (7)KUTOSIMAMA KTK MAOMBI ILI KUTAFUTA UWEPO WA MUNGU..!, 

Mtumishi Alex
Mungu atusaidie sana kuishi katika hayo ili tutangaze msimamo wa wokovu wetu, zaidi tuombe ROHO MTAKATIFU atusaidie Matendo 1:8( Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. )

BY MTUMISHI ALEX.

Comments