USHUHUDA: MAJANGA MABAYA YALITUANDAMA FAMILIA NZIMA KISA KULIKUWA NA WATU AMBAO WALITAKA NDOA YETU IVUNJIKE.

Mke wa Moses Katindasa baada ya kuangushwa na mapepo.
Bwana YESU asifiwe !
Mwaka jana mwezi wa 12 nilipatwa na matatizo mengi sana sana , tatizo la kwanza lilikuwa ni kuumia kwa mwanangu wa miaka 6 aliyekuwa anasoma shule ya chekechea pale yombo dova KKKT alipokuwa shule aliangukiwa na spika ambazo zilikuwa zinatumika kwenye mkutano wa injili hapo kanisani, walimu walimchukua wakampleka hospitali akatibiwa majeraha yalikuwa kama hizo picha zinavoonyesha. 


Baada   ya kama siku tano baada ya mtoto kuumia mimi siku hiyo niliwahi kurudi nyumbani ambapo nilimkuta mama watoto anaoga .

 Nilimwita ili niongee nae lakini nilimwona mwenzangu hana muda na mimi nikamwita kwa sauti ya upole akaja akaketi kwenye sofa , nikamuuliza kuna nini mama.  akaiambia ''asubuhi wewe ulipoondoka kuna nyoka mkubwa alinitokea hapo nyuma kanimbia 3,3,3'''  aliposema hivo akaanza kulia , nikamwambia twende kansani , tukaenda kanisani nikamkuta mwinjilisti wakati tunaendelea kumweleza mwinjilisti , mara mwinjilisti akasema huyu mbona ana pete kwenye kidole basi hapo akaanguka chini . 

Tulimwomba MUNGU sana pale baadae wale mapepo wakasema wanaondoka . basi mimi nikarudi nyumbani na mke wangu alikuwa amechoka sana nikampleka hospitali akawekewa drip akatoka ,kesho yake mimi nikaenda kazini kama kawaida saa nne nikampigia simu tukaongea vizuri lakini saa sita nilipompigia simu akaniambia nisimtafute tena yeye yupo bahari ya shamu, nilipata shida sana nikapiga simu nyumbani niaambiwa watoto amewaacha ameaga anakwenda dukani , nikampigia simu mchungaji nikamwambia kuhusiana na hii akanitia moyo , basi nikachukua pikipiki nikarudi mpaka kanisani tuliomba mpaka kama saa kumi na mbili jioni ndipo mwanaume ambae alijitambulisha kwa jina la mwalami anaefanya kazi kwenye boti ya azam akasema huyu mtu mnampigia simu yupo kwenye boti anahangaika tu nikamuomba anisaidie kumpandisha boti lakini yeye alisema anajua anakokwenda ! 

Basi mimi ikabidi nimpigie simu dada yake ambaye anaishi Zanzibar  ili amfuate, Baada ya mke wangu kufika zanzibar dada yake alimtafuta na kwa bahati nzuri akamkuta yupo kwenye uwanja wa mpira karibu na Malindi akiwa na mfuko wake wa Rambo ndani kuna udi maji ya malashi pamoja na ubani ambavyo vilikuwa ndio chakula chake.

Baada ya hapo dada yake alinipigia simu mimi akaniuliza mbona mdogo wake amekimbilia huko nikamueleza tatizo lote na nikamshauri aende nae kanisani wala asimpleke kokote , dada yake alinielewa akaenda nae efatha wakamuombea akarudi nae kwake ila anasema ilipofika saa nane usiku mdogo wake aliamka akamwambia muda wangu wa kwenda kufanya kazi yangu umefika! dada mtu akamuamsha dada mmoja mwana maombi akamwambia wakamsihi MUNGU,  akatulia kesho yake mimi nikampigia dada mtu simu ampandishe boti pamoja na mtu wa kumsindikiza na mimi sikwenda kazini kwa ajili hiyo dada yake akafanya hivyo na mimi nikampokea kama saa tano na nusu hivi pale bndarini nikamchua nikaenda nae kanisani moja kwa moja , tulipofika kanisani tukamkuta mwinjilisti na wana maombi tukaendelea kuomba mpaka jioni wakatuluhusu twende nyumbani .kesho yake mimi nikaenda kazini ila ilipofika saa saba nikasikia tena wife amelipuka mapepo ila sasa akakimbilia kanisani yeye mwenyewe kufika pale wakaomba akaanguka akaumia kichwa kama picha inavyoonyesha basi nikaenda nae hospitali wakamsaafisha akawekewa drip nikarudi nae nyumbani hali hii ilienda kama muda wa mwezi mmoja ndipo niliposhauliwa nimtafute muombaji wa mapepo, MUNGU ni mwema mama mmoja nasali nae pale kkkt akanitafutia minjilisti mmoja anaitwa mwinjilisti Ngochero yupo mkuranga akaja tukafanya maombi.

 Kesho yake wife akaanza kutapika mavitu ya ajabu sana sana kilichofuata tuliendelea katika maombi kwa muda wa wiki mbili nikamua kumpeleka kwa mama yake pale Kawe alikaa hapo baada ya wiki siku 1 jioni akaniambia hali yake ni mbaya tena nikamwambia mwambie YESU akafanya hivo akatapika tena kitu cheusi baada ya hapo vita ikahamia kwangu nilipatwa na vitu vya ajabu vilikuwa vinashika mgongo na shingo na miguu huwezi hata kuinuka ila nilimsihi MUNGU na mtumishi mmoja anaitwa Philipo wa Safina pamoja na mtumishi Peter Mabula na YESU MBINGUNI ANAENDELEA kufanya miujiza kwangu na naamini huu ndio ulikuwa wito wangu kwa MUNGU maana aliyekuwa anafanya yote haya mwisho wale mapepo walimtaja maana wife siku moja nikiwa nyumbani kwangu pale chatembo majira ya usiku kama saa tano alipandisha pepo nami nikamsihi MUNGU akanijibu kwa moto na wale pepo wakasema hata kilichokuwa kinafanya wanakuwepo pale na mtu aliewanuiza wao kuwepo na lengo lao mimi nisiishi na mke wangu namshukuru MUNGU BABA , MWANA  na ROHO MTAKATIFU nipo salama mpaka leo maana nilipokea hata vitisho kutoka kwa hao wahusika lakini siwezi siwezi kuwa msiri maana MUNGU anaona yaliyo sirini ni kweli nilipelekwa kwa mganga wa kienyeji na huyo mama na huyo mzee maana mwanzo niliishi nao kama wazazi wangu na ni wao ndio walinishauri hata mimi kwenda kwa mganga wa kienyeji Enzi hizo mpaka nilithuhbutu hata kuvaa pete ya kujikinga ila niliambulia mateso makali pamoja na ndoto mbaya kila siku, Lakini BWANA YESU amenihurumia na sasa naendelea vizuri.

MUNGU awabariki sana na tuombeane siku zote.
Mtoto wa Mose baada ya kuangukiwa na spika.
mtoto wa Moses Katindasa
Na BWANA YESU atatengeneza nja pasipo na njia.

Moses Ktindasa

Comments