WOKOVU KWANZA *sehemu ya kwanza *

Na Mtumishi Gasper Madumla


Imeandikwa:
" Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake.
Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri.
Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo. Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. " Luka 19:1-3,10

Bwana Yesu asifiwe...
Nasema,Haleluya...
Ooooh...
Blessed be the name of Jesus,
Say;
AMEN...

Siku ya leo,kazi yangu ni ndogo tu,na wala sina kazi kubwa sana,bali nina kazi ya kukuwekea msingi wa fundisho hili zuri lililoanza siku ya leo katika muda sahihi,na wakati sahihi kabisa.

Biblia inasema kwamba,Zakayo alikuwa ni mtu tajiri mwenye kufanya kazi ya ushuru,kwa leo Zakayo tungeweza kumuita ni mkurugenzi mmojawapo/boss wa TRA.
Sasa upate picha ya kwamba mtu wa namna hii ndio anatafuta amuone Yesu,pata picha hiyo.
Au pata picha hii;
Chukulia leo,Bwana Yesu anaingia mjini Dar-es salaam,kisha ndani ya Dar,anakuwepo mtoza ushuru mmoja mwenye kutafuta kumuona Yesu.

Haleluya...

Ikumbukwe kwamba,yule mwenye kumtafuta mtu,ni lazima atakuwa amemsikia habari za mtu huyo amtafutaye.
Hivyo hata Zakayo naye,alipata kusikia habari za Bwana Yesu,ndiposa akatafuta kumuona ni mtu wa namna gani,
Kama Zakayo alipata kusikia habari za Yesu Kristo,basi Zakayo aliamini ingawa alikuwa ni mdhambi tu wa kawaida.

Zakayo alikuwa na kiwango fulani cha imani,sababu alipata kusikia habari za Bwana Yesu,sababu IMANI chanzo chake ni kusikia,tunasoma;

" Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. " Matendo 10:17

Sisi watu wa leo kama tutasikia neno la Kristo,basi ni dhahiri tutakuwa na shauku ya kumtafuta Bwana Yesu kwa hali na mali yoyote ile kama alivyofanya Zakayo. Na kwa kupitia hapo ndipo tutakuwa wakristo kweli kweli.
Sababu yeye anayesikia neno huwa ni mtendaji wa neno.

Shida kubwa tuliyokuwa nayo kanisa la leo,
Hatusikii neno la Kristo,
• Na ndio maana hatuna njaa ya kutenda mema.
• Na ndio maana hatuna shauku ya kumtafuta Bwana Yesu kwa dhati kabisa,tazama jinsi ilivyokuwa kwa Zakayo,alipoona haitoshi akaamua kupanda juu ya mkuyu.

Haleluya...

Biblia inatupa sababu mbili ambazo zilimkwamisha Zakayo kutomuona Bwana Yesu,Sababu hizo zimewekwa wazi kabisa kwamba;
• UMATI wa watu ulimkwamisha Zakayo kushindwa kumuona Bwana Yesu. Lakini pili ni;
• UFUPI WA KIMO,Zakayo alikuwa ni mfupi wa kimo hata hasiweze kumuona Yesu.

Sababu hizo mbili zilikuwa zinamkwamisha Zakayo kumuona Yesu,ingawa Zakayo alitamani sana aonane na Bwana Yesu,
Sijui sababu zilizopo kwako wewe mpendwa wangu usomaye sasa,zile zenye kukukwamisha kumuona Bwana Yesu.

Yamkini yawezekana umati wa watu unakukwamisha usikutana na Bwana,
Au,
Yamkini U mfupi wa kimo kwa habari ya mambo ya kiroho. Sijui ufupi wako upo wapi?
Lakini jambo moja ninalolijua siku ya leo ni kwamba Yesu Kristo atakuhudumia siku ya leo,mahali hapa hapa,na utakutana na Bwana,ni kuamini tu haya nikuambiayo.

01.UMATI WA WATU KAMA UKUTA.

Hii ni moja ya sababu iliyomzuia Zakayo kuonana na Bwana Yesu Kristo.
Siku zote umati wa watu huwa kama ukuta ukuzuiao kukutana na Mungu.Nasema UMATI WA WATU wala sio shetani.
Labda tazama hata jinsi ilivyokuwa kwa Bartimayo yule aliyekuwa kipofu,Biblia inatuambia hivi;

" Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu.
Na wengi wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupaza sauti, Mwana wa Daudi, unirehemu. " Marko 10:47-48

Bartimayo alikemewa na wengi ili anyamaze kabisa,hawa waliomkemea Bartimayo ni UMATI WA WATU ambao hawakutaka kabisa kuona Bartimayo anapokea uponyaji wake.

Lakini cha ajabu ni kwamba;
Umati wa watu hawa ndio waliokuwa wakitembea na Yesu katika msafara mmoja,Ndiposa nikajifunza jambo moja kwamba,
Wapo watu wanaotembea na Yesu lakini hawana Yesu mioyoni mwao.Watu wa namna hii wapo wengi makanisani mwetu,na kamwe hawawezi kukupa mwanya wa kupokea muujiza wako

Je unajua;
• Wale wote waliomkemea Bartimayo anyamaze kwa hila zao mbaya,ndio hao hao waliombeba Bartimayo na kumpeleka kwa Bwana Yesu.
Maana Bwana Yesu aliwaambia,mwiteeni...

Nami nakutangazia siku ya leo kwamba,wale wote wenye kuzuia mafanikio yako,ndio watakusaidia kufanikisha mafanikio yako katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti,POKEA...Sema AMEN.

Watu hawapendi kukuona unafanikiwa kwa jambo lolote lile,ni lazima wakukinge kinge na kukukemea unyamaze.
Mpendwa,uonapo makemeo juu ya IMANI yako kwa Bwana Yesu,kamwe usinyamaze hata kidogo maana ushindi wako upo hapo. Laiti kama Zakayo au Bartimayo wangenyamaza,basi wasingepokea majibu yao.

Marafiki wako pia wanaweza wakafanyika kuwa kama UMATI WA WATU wenye kukuzuia kuuona ufalme wa Mungu.
Wapo watu chini ya jua hili,wenye kuwapenda na kuwaogopa sana rafiki zao hata kufanya na kuyafuata mambo wayafanyao hao marafiki zao hata kama ni machukizo mbele za Bwana Mungu. Wengi hufanya maovu kwa kuwapendezesha wanadamu wenzao na si Mungu.

Leo hii watu wengine makanisani wameshashuhudiwa na Mungu Baba kwamba watoke,waokoke na kwenda kuabudu sehemu nyingine sawa sawa na maelekezo ya Roho mtakatifu,lakini cha ajabu hawatoki kwa sababu wanawaonea haya UMATI WA WATU makanisani mwao,kwamba wakitota na kuokoka watu watawaonaje?

Zakayo alisongwa sana na umati wa watu wenye hila mbaya na wachache sana wenye nia nzuri....

ITAENDELEA....

• Kwa huduma ya maombi na maombezi,tafadhali piga namba yangu hii;
0655111149.

• Usikose fundisho hili zuri!

UBARIKIWE.

Comments