WOKOVU KWANZA *sehemu ya pili *

Na Mtumishi Gasper Madumla


" Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake.
Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri.
Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo. " Luka 19:1-3

"Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. " Luka 19:10

Haleluya...
Bwana Yesu asifiwe....

Kumbuka jambo moja la msingi nililokuambia katika sehemu ya kwanza,kwamba kilichomzuia Zakayo asimuone Bwana Yesu,ilikuwa ni UMATI WA WATU ambao ulimsonga songa,Umati huu ulikuwa kama ukuta kwake.

Mara nyingi watu wengi tunashindwa kufanya vizuri kwa sababu tunawatazama watu.
*Umati wa watu huzuia mtu asiokoke na kumjua Bwana Mungu wake.
*Umati wa watu huzuia muujiza,
*Umati wa watu huzuia mtu asifike pale alipokusudia afike.N.K

Mpendwa naomba uwadharau watu,kufanikiwa kwako ni kudharau macho ya watu,Nasema wacha wakuseme kwamba U mjinga kwa habari ya mambo ya ufalme wa Mungu,lakini cha msingi ujue nini unafanya,sababu wao wakusemao hawana maisha,maisha mwenye nayo ni mmoja tu,maisha halisi yapo kwa Yesu Kristo wa Nazareti,WOKOVU KWANZA ,
Imeandikwa kwamba ;

"Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu..." Matendo 17:28

Na zaidi ya hapo,tunatakiwa tugeuzwe kuwa kama watoto kwa habari ya dhambi,
Tunasoma;
" Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima. " 1 Wakorintho 14:20

Biblia inatuambia katika uovu tugeuzwe kuwa kama watoto wachanga,lakini tuwe watu wazima katika akili.

Mimi binafsi nilipokuwa huko duniani(nilipokuwa SIJAOKOKA),nami pia naliogopa UMATI wa watu,kwamba eti niende kuokoka,nilikuwa nikijiuliza nikiokoka itakuwaje? Watu watanionaje?Watu walikuwa ni kama ukuta kwangu,

Lakini ilipofika wakati wa Bwana uliokusudiwa,nikakata shauri,Bwana akaniokoa,nikaokoka. Nami nataka nikutangazie siku ya leo,kwamba TANGU NIOKOKE MPAKA SASA,SIJAWAHI KUPATA HASARA YOYOTE ZAIDI YA KUPATA FAIDA.

Watu walimzuia Zakayo,lakini Zakayo akapiga hesabu kubwa na ni kama vile anasema hivi ;
"ikiwa watu wamenikinga,je ni kweli kabisa niishi pasipo kumuona Yesu?,hapana lazima nichukue hatua mbadala...." Ndiposa tunamuona Zakayo akipanda juu ya mkuyu kwa lengo la kumuona Bwana Yesu.

Kutowaogopa watu haitoshi,yakupasa kuchukua hatua madhubuti ya kupanda mkuyu ili uonane na Bwana Yesu. Kwa lugha nyingine ni kwamba ili uonane na Bwana Yesu ni lazima ufanye maamuzi magumu;
Kwanza ukate shauri,
Usiwaangalie watu wanakuonaje,wala wanakusemaje,lakini pili;
Ni kwenda kwa Yesu mahali alipo.

Haleluya,..

Hivi unafikirije?
Kama Zakayo angelipanda Mkuyu wowote ule ambao Yesu hayupo,Je angeliweza kuonana naye?

Jibu;
Zakayo kama angelipanda Mkuyu wowote ule asingelionana na Bwana Yesu.

Bwana Yesu asifiwe...
Oooh... Haleluya....

Maandiko tuliyoyasoma hapo juu kabisa ( Luka 19:1-3,10) yanatueleza sababu mbili zilizomzuia Zakayo kuonana na Yesu.
(Sababu ya kwanza kama tulivyoiangalia ambayo ni kusongwa na watu)
Sababu ya pili biblia inasema kwamba ni. UFUPI WA KIMO.

02.UFUPI WA KIMO.
Laiti kama Zakayo hasingelikuwa mfupi wa kimo,basi angeliweza kumuona Yesu wa Nazareti kwa wepesi zaidi. Lakini kwa sababu alikuwa mfupi wa kimo,watu wakamkinga,na kumsonga songa na hatimaye hakuweza kumuona Bwana Yesu.

Ufupi wake Zakayo ulikuwa umesongwa na umati wa watu,maana kama watu wasingelikuwepo basi Zakayo angeliweza kuonana na Bwana Yesu kwa urahisi hata kama ni mfupi wa kimo cha namna yoyote ile.

Sasa,Biblia inatufundisha jambo kubwa la msingi la maisha yetu ya IMANI pale inavyotuambia habari ya ufupi wa Zakayo

Kwa habiri ya mambo ya imani, ufupi wa kimo ni ile IMANI iliyosongwa na vitu au mambo ya kidunia hata kushindwa kuonana na Bwana Yesu,na hiyo ndio tafsiri sahihi ya ufupi wa kimo kiimani.

Mfano mzuri;
Ndani yake Zakayo alinia kumuona Yesu,maana alijua atapita njia ile,sasa kwa sababu ya watu waliomsonga songa ambao watu hao ni walefu kuliko yeye,wakamzuia asimuone Yesu Kristo masiya.
Leo hii,unaweza ukawa mmoja wa mtu mwenye kutafuta kumuona Yesu,lakini kwa ufupi wa Imani yako ILIYOSONGWA SONGWA NA WATU WAKO WA KARIBU ukashindwa kumuona Yesu.

Haleluya...

• Jambo moja unalotakiwa kufanya ni kuthubutu kuchukua hatua ya dhati kwa kungangana kumuona Yesu Kristo hata kwa gharama yoyote ile pale unapogundua kwamba umesongwa na watu wasioamini.

Lakini pia tunaweza kuangalia jambo hili kwa mtizamo mwingine,kwamba Ufupi wa kimo ni upungufu fulani hivi wa IMANI uliosongwa na mambo ya kidunia ambao upungufu huu humfanya mtu kushindwa kufikia sehemu fulani iliyohitajika ufike.Zakayo,ingawa alitamani sana amuone Yesu,lakini ufupi wake ukamzuia maana yake kama asingelikuwa mfupi wa kimo basi,angelimuona.

Kama ndio hivyo basi;
Kiimani ninaweza sema kwamba ufupi wa kimo unafananishwa na upungufu wa Imani,imani inayoshindwa kumuona Bwana Yesu. Imani iliyopungua sehemu fulani ambayo mara nyingi haina majibu wala matokeo yoyote yale. Kama una kumbuka hii, wanafunzi wa Yesu nao walishindwa kufanya huduma ,kwa sababu ya;
• Upungufu wa imani,
Imeandikwa;

" Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa?
Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. " Mathayo 17:19-20

( Sababu nyingine iliyo wakwamisha ni kushindwa kufunga na kuomba) Mathayo 17:21.

Haleluya....

ITAENDELEA...

• Kwa huduma ya maombi na maombezi wasiliana nami kwa namba yangu hii 0655111149.
• Usikose kabisa fundisho hili.

UBARIKIWE.

Comments