ZIFAHAMU KARAMA ZA KIROHO NA KARAMA BANDIA.

Na Mtumishi Alex
(A)"KARAMA ZA KIROHO": Karama za kiroho zinajulikana kama karama za kiroho kwa sababu chimbuko lake ni ROHO MTAKATIFU.
 ROHO MTAKATIFU ndiye anayetenda kazi kwa kila karama. "1KOR 12:4-11" Hapa biblia inaeleza kuwa kuna tofauti ya karama lakini Roho ni yule yule mmoja atendaye kazi kwa kila karama. 

Biblia inaeleza Huduma za ROHO MTAKATIFU kama ifuatavyo-: "WAEFESO 4:11-12" hapa kuna karama kama vile, 
UTUME, 
UNABII, 
UINJILISITI, 
UCHUNGAJI, na 
UALIMU.

 Pia biblia inataja karama zifuatazo "1KOR 12:8-10" kuna karama kama vile 
 NENO LA HEKIMA, 
NENO LA MAARIFA,
NENO LA IMANI,
 KARAMA YA KUPONYA,
 MATENDO YA MIUJIZA, 
 KUPAMBANUA ROHO, 
AINA ZA LUGHA, 
TAFASRI ZA LUGHA, 
 Hizi zote ni karama za kiroho na ROHO MTAKATIFU ndiye anayetenda kazi ktk karama hizi.

 (B)KWA NINI KARAMA ZA KIROHO ZINATOREWA? Karama za kiroho zinatolewa kwa sababu zifuatazo:- 

(1)KUWAKAMILISHA WATAKATIFU-->"WAEFESO 4:12 Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke hata mwili wa Kristo ujengwe.

 (2)KUJENGA WATU WA MUNGU-->"1KOR 14:4, 12 Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake, bali ahutubuye hulijenga kanisa. mstari wa 12 anasema, Hivyo hivyo na ninyi kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni sana kwamba mzidi kuwa nazo ili kulijenga kanisa

 (3)KUWAANDAA WATU WA MUNGU KUZIKABILI SIKU ZA USONI KWA UHAKIKA NA KWA AJILI YA UZIMA WA MILELE-->"WARUMI 6:23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele ktk KRISTO YESU BWANA wetu.. Lakini pamoja hayo yote Lengo la karama za kiroho kutoa mawasiliano kati ya Muumba na viumbe vyake. --SOMO HILI-- Litaendelea, usikose sehemu ya mwisho ambapo tutaangalia KARAMA BANDIA. 
Barikiwa!
 By Mtumishi Alex

Comments