BABY MADAHA AMGEUKIA MWENYEZI MUNGU

  Staa wa filamu Bongo Baby Joseph Madaha
  
Kufuatia vifo vya wasanii vilivyotokea mfululizo, mwigizaji Baby Joseph Madaha amelazimika kubadili mtindo wake wa maisha na kuishi kitakatifu.
 
Akipiga stori na wana habari,  Baby  Madaha alisema anawasihi hata wasanii wenzake wabadili mfumo wa maisha kwa kumgeukia Mungu na kufanya ibada kila mara kwa kuwa vifo hivyo vinawapa somo la kuwakumbusha kumkaribia Mungu.

“Nimebadili mfumo wa maisha kwa kufanya ibada na ninawashauri wasanii wenzangu  tumgeukie Mungu kwani vifo na mambo yanayotokea yanatukumbusha ibada na kujiweka safi,” alisema Baby Madaha.


Kutoka kwa blogger.

MUNGU awasaidie hawa wanaojiona kuwa ni watu maarufu maana umaarufu wao ni hapa hapa duniani, mbinguni hakuna anaowajua. Wanazidiwa umaarufu na watoto wadogo ila tu wanaisha maisha ya kumpendeza MUNGU huku wamempa BWANA YESU maisha yao.

Sio mpaka matatizo yaje ndio tumkumbuke MUNGU lakini wakati wa amani tunamsahau MUNGU kama yupo.

WOKOVU NI SASA NA KAMA SIO SASA BASI NI SASA HIVI.
 
 
 

Comments