BARAKA JANGWANI

Na Frank Philip


"Nunueni vyakula kwao kwa fedha, mpate kula; na maji nayo nunueni kwao kwa fedha, mpate kunywa. Kwa kuwa BWANA, Mungu wako, amekubarikia katika kazi yote ya mkono wako; amejua ulivyotembea katika jangwa kubwa hili; miaka arobaini hii alikuwa nawe BWANA, Mungu wako; hukukosa kitu" (Kumbukumbu la Torati 2:6,7).

Jangwani sio mahali pa zuri, ni mahali pa kupungukiwa, mahali pa kiu na adha nyingi; ila JANGWA limekuwa shule nzuri kwa wengi. Mungu amejitukuza katika udhaifu wetu na kupungukiwa. Uaminifu wake umekuwa dhahiri kwa maana tumetambua kwamba hata katika JANGWA hatutaona kiu; hata NYIKANI hatutana njaa. Jua halitatupiga wakati wa mchana, wala mwezi wakati wa usiku, Mkono wake utatufunika na kutulinda, naam, japo ni JANGWANI, tutaona baraka za Mungu wetu na kumshukuru.

Basi na tuwe na moyo wa hekima ili tusifie JANGWANI kwa maana hapo sipo petu. Mungu hakutukusudia KUTESEKA na KUUMIA siku zote. Tukiisha kupita JANGWANI, na NYIKA isiyo na maji na chakula cha kutosha kwa UAMINIFU na UELEKEVU mbele za Bwana Mungu wetu, HAKIKA tutavukia nchi iliyojaa MAZIWA na ASALI.

Ona jambo hili, Mungu huwapumzisha watu wake, huwapa burudani. Jangwani ni mahali pa kupita tu, iko siku inakuja, Mungu atakuondolea adha zako na msiba wako, ILA imekupasa KUMSTAHI mbele za adui zake, na KUMHESHIMU Mungu upitapo JANGWANI ili usimkasirishe na KUJIKOSESHA mambo mema akuwaziyo mbele zako. Mshukuru Mungu katika shida na raha kwa sababu hayo ni mapenzi yake kwako, sawa, inauma, huelewi kwa sasa, ila UKIISHA kuvuka, utatambua Mungu alikua nawe na hakukuacha wala kukupungukia.

Usitende dhambi, usirudi nyuma, mtumaini Mungu wako ni mwaminifu. Yeye sio mwanadamu hata aseme uongo, alicho ahidi atatenda.

Frank Philip.

Comments