![]() |
Dk. Rudi Zimmer wa chama cha Biblia Brazil akifafanua juu ya maono haya ya Chama Cha Biblia ambayo yamefanikiwa. |
Chama cha
Biblia cha Brazil kimesambaza Biblia mioni tano(5) katika jitihada zake za
kuyafikia mamilioni ya watu walioingia nchini humo kutazama mashindano ya kombe
la dunia.
Viongozi wa
shirika hilo la kimataifa wamesema hawawezi kuyaacha mashindano hayo yapite
hivi hivi bila wati kulijua neno la MUNGU.
Makisio ya
shirikisho la mpira wa mguu duniani(FIFA) ni kwamba wageni zaidi ya milioni 1.5
wangeingia Brazil kwa ajili ya kushuhudia fainali hizo.
Pamoja nao,
chama cha Biblia Brazil kilikisia kwamba wabrazil milioni3 wangeshiriki
viwanjani kutazama mashindano hayo na hivyo wakatenga Biblia za kutosha kwa ajili yao.

Maisha ya
ushindi blog tunapongeza sana maono yaka ya chama cha Biblia cha Brazil.
Mbali na
usambazaji wa Biblia hizo, nakala 20,000 za vitabu vya injili ya Yohana
zitasambaza kwa lugha ya kireno pamoja na lugha zingine 7 za mataifa
mbalimbali. Pia chama hicho kimechapisha matoleo ya Agano jipya na agano la
kale yanayosambazwa kwa watazamaji.
Katika
kufanikisha uinjilisti huo chama cha Biblia Brazil, makanisa 1,600 na mamia ya
huduma za kiinjili nchini Brazil wameungana kugawa maandiko haya. Harakati hiyo
ya kugawa maandiko matakatifu imepewa jina la FAIR PLAY BRAZIL.
Maandiko
hayo ya neno la MUNGU hugawiwa wakati watazamaji wakijiandaa kuingia katika
viwanja vya miji 12 vinavyotumika kwa ajili ya mashindano hayo.
Kombe la
dunia 2014 limeanza tarehe 12 june 2014,
katika uwanja wa sao Paulo, ambapo timu za taifa 32 duniani zinashiriki.
MUNGU
awabariki sana chama cha Biblia cha Brazil.
![]() |
Baadhi ya maandiko ya Biblia ambayo yana kava ambazo zinaonyesha miji 12 ambayo inaandaa kombe la dunia 2014. |
Comments