![]() |
Na Mwinjilisti John Chinyuli |
kuna watu wengi mno ambao wameshakufa na wengine wengi wako mahututi kwasababu hawakufanya maamuzi yenye nidhamu na msimamo ndani yake juu ya maisha yao kwa habari za kuacha dhambi mpaka wakaja kufa huku hizo dhambi zilizo kuwa zikiwasumbua zikawaua (watakuta zimewatangulia zinawasubiri)na hilo tu nikwasababu ya kukosa nidhamu na msimamo wa maamuzi na kuwa na Mizaha na michezo michafu.
dhambi inayokusumbua usipoifanyia maamuzi ya kufa mtu ama zake ama zako ,kimoja lazima kife kama siyo wewe ikuue,basi wewe uwahi uiue dhambi kwenye maisha yako ukichelewa yenyewe itakumaliza itakufuta kabisa na kumbukumbu yako duniani haitakuwepo,
dhambi inahitaji maamuzi yakinifu yasiyo na mizaha ndani yake pasipo kuona soni wala kuangalia wengine wanafanya nini huku Mungu akiwa upande wako,si ajabu sana kuona mtu akikiri kabisa na kuapiza kuwa hatakuja kurudia ushetani fulani lakini gafla unashaanga karudi tena nyuma huwa najiuliza ni nini kimetokea hapo kumbe hakuwa na nidhamu na maamuzi yake wala msimamo kwa kile alichokiamua ndani yake,Ninaposema dhambi inakuua isipokuua kimwili itaua furaha ya maisha yako,ama uchumi wako,ama elimu yako,ama ndoa yako,ama afya yako,ama maono yako.....
FANYA MAMBO YAFUATAYO KUSHINDA(kuua) DHAMBI YOYOTE INAYOKUSUMBUA NA KUTESA MAISHA YAKO
-Soma na tafakari neno la Mungu kila iitwapo leo
-Funga na kuomba ili kuutiisha mwili na kuipa roho nguvu
-Jitenge mbali na makundi mabaya
-Acha mizaha
MUNGU akubariki sana.
By Mwinjilisti John Chinyuli
0767 592989/0712 592989
Comments